Friday, April 4, 2014

MATUKIO YA BARABARANI JIJINI DAR LEO KATIKA PICHA


 Ujenzi wa Barabara za mabasi yaendayo kasi ukiendelea jijini Dar es Salaam, hapa ni eneo la Mkwajuni mafundi wakiendelea na ujenzi wa njia hiyo ya mabasi.
 Gari la taka lenye namba za usajili T 889 APV, likiwa limeanguka katika barabara ya Bagamoyo eneo la Kawe Bondeni karibu na daraja linaloendelea kujengwa leo asubuhi. Haikuweza kufahamika kwa haraka chanzo cha ajali cha gari hilo lililokuwa limesheheni Taka na kusababisha foleni kubwa mida ya asubuhi.
 Magari yakianza kutembea baada ya kuruhusiwa na kuzuiliwa ya upande mmoja kutokana na ajali hiyo.
 Muonekano wa Barabara Magomeni eneo la Bonde la Mkwajuni kabla ya kuanza kubomolewa.
 Hii ni barabara ya Bagamoyo eneo la Mwenge ikiwa imetuama maji eneo la katikati ilipoachwa rizevu ya njia ya mabasi yaendayo kasi itakayotengenezwa siku zijazo.
 Hebu ona madereva hawa wa Bajaji mida ya asubuhi wanavyokera, pande zote wamekaa wao na huku hawatembei mwendo unaotakiwa na kusababisha foleni ya magari yaliyo nyuma yao, huku wakiwa wameachagepu kubwa mbele yao. 

Madereva walio wengi wanahitaji kupata elimu ya matumizi ya barabara, kwani unamkuta dereva anaongea na simu na anatembea mwendo wa speed 20, lakini amekaa upande wa kulia badala ya kukaa kushoto na kuwapisha  waendao speed wapite upande huo wa kulia.

No comments:

Post a Comment