Saturday, September 7, 2013

BOFYA HAPA NYIMBO MPYA YA DIAMOND-MY NUMBER 1

KUNANI JUSTIN BEIBER NA PARIS JACKSON

Baadhi ya watu wajiuliza ukaribu wao

*STARS YAWASILI BANJUL, KUIVAA GAMBIA LEO



Na Boniface Wambura, Banjul +2207362384
Kikosi cha Taifa Stars kimewasili salama hapa Banjul, Gambia tayari kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya wenyeji itakayochezwa leo Septemba 7.

Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imewasili hapa jana (Septemba 5 mwaka huu) saa 11 jioni ikitokea Dakar, Senegal ambapo ilichelewa kuunganisha ndege, hivyo kuamua kutumia usafiri wa barabara kwa vile ni karibu na baadaye kupanda kivuko kuingia Banjul badala ya kulala na kuchukua ndege nyingine siku inayofuata.

Wachezaji wako katika hali nzuri na leo jioni wanatarajia kufanya mazoezi ya mwisho kwenye Uwanja wa Independence ulioko Bakau ambao utatumika kwa mechi ya kesho. Timu imefikia hoteli ya Seaview iliyoko kandokando ya Bahari ya Atlantic.

Mechi hiyo itaanza saa 10.30 jioni kwa saa za hapa ambapo nyumbani Tanzania itakuwa saa 1.30 usiku, na itachezeshwa na waamuzi kutoka Rwanda Munyemana Hudu. Waamuzi wasaidizi ni Theogene Ndagijimana, Honore Simba na Issa Kagabo. Kamishna ni Andy Quamie kutoka Liberia.
Washabiki na vyombo vya habari vya hapa wanaizungumzia mechi hiyo ambayo ina umuhimu mkubwa kwa pande zote, huku Gambia ikiwa imeita wachezaji tisa wanaocheza barani Ulaya na Marekani. Gambia ambayo imepata uongozi mpya wa Chama cha Mpira wa Miguu Gambia (GFA) imepania kuhakikisha haimalizi mechi za mchujo ikiwa na pointi moja tu.

Kwa upande wa Tanzania, Kocha Kim Poulsen amesema nia ni kuona Stars yenye pointi sita inamaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Ivory Coast ambayo tayari imechukua tiketi pekee ya kucheza raundi ya mwisho kutoka kundi hili la C.

“Mechi hii ni muhimu kwetu kwa vile tunataka matokeo mazuri ugenini. Lakini kikubwa ni kuwa matokeo mazuri si tu yatatuweka katika nafasi ya kuwa wa pili, lakini vilevile yatatusaidia kuongeza pointi kwenye viwango vya ubora vya FIFA, na kikubwa zaidi hii ni sehemu ya maandalizi ya sisi kucheza Fainali za Afrika za 2015,” amesema Kim.

Stars inatarajiwa kupangwa hivi; Juma Kaseja, Vincent Barnabas, Erasto Nyoni, Nadir Haroub, Henry Joseph, Frank Domayo, Haruni Chanongo, Amri Kiemba, Mrisho Ngasa, Simon Msuva na Khamis Mcha

*REDD'S MISS TANZANIA 2013 WATEMBELEA RADIO 5 YA JIJINI ARUSHA



Mtangazaji wa kipindi cha burudani cha Funika Base kutoka Radio 5 ya Mjini Arusha , Julius Kamafa (kushoto) akifanya mahojiano na Washiriki wa Shindano la Redd’s Miss Tanzania 2013 katika studio za redio hiyo jana.
 Baadhi ya warembo wakijieleza Live Redio 5 hii leo walipotebelea kituo hicho. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPO CHINI

FIESTA KUWASHA MOTO MBEYA.



Msanii wa muziki wa kizazi kipya,ambaye kwa sasa anafanya vyema kwenye anga za muziki huo,Neylee akiimba kwa hisi jukwaani huu wakati tamasha la Serengeti Fiesta likiendelea kwa shangwe ndani ya uwanja wa Sokonine.
Wakazi wa jiji la Mbeya wakiwa wamejitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013 ndani ya uwanja wa Sokoine,ndio kwanza shoo inaanza ambapo msanii aliyewahi kuiwakilisa shindano la BSS,Walter Chilambo ndiye aliyefungua pazia la onesho hilo usiku huu. 

 Tamasha la Serengeti Fiesta 2013 likiendelea usiku huu kwenye uwanja wa Sokoine,Mkoani Mbeya
 Mama wa miduara ya Kibongofleva,Shilole akiwa na madensa wake wakitumbuiza jukwaani usiku huu ndani ya tamasha la Serengeti fiesta 2013,ndani ya uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPO CHINI