Friday, June 28, 2013

*WAWILI WACHAGULIWA KITUO CHA VIPAJI ASPIRE


Wachezaji wawili kutoka Tanzania ni miongoni mwa wachezaji 50, waliochaguliwa baada ya kufanyiwa majaribio nchini Uganda kwa ajili ya kuingia katika kituo cha kuendeleza vipaji (centre of excellence) kilichopo Doha nchini Qatar, kupitia mpango wa kukuza vipaji wa Aspire Football Dream.
Wachezaji hao ni pamoja na Abdulrasul Tahir Bitebo (15) ambaye ni mshambuliaji kutoka Kituo cha Uwanja wa Karume, na Martin Omela Tangazi (14) ambaye ni beki kutoka Kituo cha Ukonga ndiyo waliochaguliwa kutoka Tanzania kuingia katika kituo ambapo watakaa kwa mwezi mmoja kabla ya kusaini mkataba rasmi wa kuendelezwa.

Wachezaji wengine walikuwa wakitoka katika nchi za Uganda na Kenya. Mchezaji mwingine aliyefuzu katika nafasi tatu zilizokuwepo ni kutoka nchini Kenya.

Mpango wa Aspire Football Dream unafadhiliwa na Mtoto wa Mfalme wa Qatar katika nchi 16 duniani, na kwa hapa nchini uko chini ya Idara ya Ufundi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

TFF ina jumla ya vituo 14 vya kuendeleza vipaji kupitia mpango huo wa Aspire Football Dream. Vituo hivyo ni Karume, Kigamboni, Tandika, Kawe, Ukonga, Kitunda, Mbagala, Magomeni, Makongo, na Tabata vilivyo katika Mkoa wa Dar es Salaam. Vingine ni Bagamoyo kilichopo mkoani Pwani, Morogoro, Arusha na Moshi mkoani Kilimanjaro.

Kituo kingine cha kuendeleza vipaji (centre of excellence) cha Aspire kipo Dakar nchini Senegal

Thursday, June 27, 2013

*FAMILIA YA MANDERA YAZUA UTATA KUHUSU NI WAPI ATAZIKIWA


Na. Halima Kambi, Dar
Bado Bara la Afrika likiwa katika wingu nzito juu ya Afya ya baba wa Afrika Kusini Nelson Mandela familia yake nayo imeingia katika utata mkubwa juu ya mahali atakapozikwa Rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini pindi atakapokufa.

Hali hiyo imejitokeza hivi karibuni baada ya mjukuu wake, Chifu Mandla Mandela kususia kikao cha familia na kutoka nje ya kikao hicho baada ya kukasirishwa na mjadala wa kufufua miili ya  watoto  watatu  wa mandele .

Kutokana na familia inataka miili ya watoto  hao Thembekile, Makgatho na Makaziwe yaamishiwe Qunu ambako Mandela atazikwa.

Vyanzo vya habari tofauti nchini humo vilisema familia hiyo ilitofautiana na Mandla ambaye anataka babu yake azikwe mahali akozaliwa Mvezo huko wengine wakitaka wosia wwake wakuzikwa karibu na wanawe uheshimiwe
Pia familia ya mzee Nelson Mandela imeanza kusafisha makaburi pamoja na kupanda maua maeneo yanayozunguka viunga hivyo ikiwa ni ishara ya kujiandaa kwa lolote litakalotokea hivi karibuni..

Familia hiyo imefanya maamuzi hayo baada ya hali ya kiongozi huyo kuendelea kutokutia matumaini tangu kupelekwa kwake hospitali kwa ajili ya matibabu

Nelson Mandela ndiye kiongozi pekee wa Afrika aliyejitoa maisha yake kwa ajili ya kupinga na kupambana na ubaguzi wa rangi dhidi ya makaburu nchini Afrika ya Kusini..

Hata hivyo maradhi yanayomsumbua kiongozi huyo hivi sasa  ni pamoja na kuathirika kwa mapafu maradhia ambayo yalianza kummaliza toka alipokuwa gerezani

Mbali na utata katika familia pia katika nyumba ya Mzee Mandela Houghton 12th Ave, waandishi wa habari kutoka nchini Marekani wameweka kambi nje ya nyumba hiyo, pia  Rais Zuma ameahirisha safari ya kwenda Mozambique.

Bado maswali mengi yapo kwa wananchi ndani ya Afrika ya Kusini na nje ya juu ya hali yam zee huyo kwani tayari wananchi wanahisi mzee Mandela ameshafariki Dunia lakini madaktari na familia inawaficha katika jambo hilo.

TUZIDI KUMUOMBEA MZEE MANDELA ILI AWEZE KUPONA MARADHI YANAYOMSUMBUA KWANI BADO AFRIKA INAMUHITAJI SANA

*RAIS KIKWETE AKUTANA NA KIONGOZI WA SHIRIKA LA UNDP BI.HELEN CLARK, IKULU LEO

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, akimkaribisha na kufanya mazungumzo na Kiongozi wa Shirika la UNDP (UNDP Administrator) Bi. Helen Clark, ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Picha na Freddy Maro.

*UCHAGUZI WA VIONGOZI WA BFT KUFANYIKA JULAI 7.


TANZANIA BOXING NEWS: UCHAGUZI BFT JULAI 7


Uchaguzi wa viongozi wa BFT uliopangwa Kufanyika tarehe 7/7/2013 jijini Mwanza, utafanyika kwa tarehe hiyo kama ulivyopangwa.

Kikao cha kamati ya utendaji ya BFT kilichofanyika juzi katika  ofisi za BFT kikiongozwa na Rais wa shirikisho Joan Minja kimesisitiza kuwa uchaguzi utafanyika kama ulivyopangwa na haujaairishwa kama baadhi ya kikundi 
cha watu wachache wanaojiita wadau wanavyoweka pingamizi na kupotosha  
kwa kuwashawishi wajumbe wa mkutanao mkuu hasa kutoka mikoani 
kutohudhuria mkutano huo wa uchaguzi,kwa manufaa yao binafsi na 
kinyume na katiba yetu.

Upotoshaji huo unafanywa na  Akaroly Godfrey aliyekuwa  kiongozi katika uongozi uliojiudhuru kutokana na kashfa za kusafirisha madawa ya kulevya 
na kusababisha Tanzania kufutwa uanachama na chama cha ngumi cha 
dunia (AIBA) na kusababisha  kutoshiriki mashindano,mikutano na 
shughuri zote za kimataifa za chama cha ngumi cha Dunia AIBA. Naomba 
wadau na serikali kuwa makini na watu wanaoshawishi kwa lengo la 
masilahi yao binafsi na kusababisha michezo kudolola badala ya kusonga 
mbele.

Fomu za uchaguzi zilishaanza kutolewa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) toka tarehe 4//2013 na zitaendelea kutolewa hadi tarehe 4/7/2013 jijini 
Mwanza na tarehe hiyo  ndio itakuwa siku ya mwisho ya kuchukua na 
kurudisha fomu, tarehe 5/7/2013 itatakuwa siku ya usaili na utafanyika jijini mwanza, tarehe 6/7/2013 kupitia pingamizi na kuzitolea maamuzi na tarehe 7/7/2013 ndio siku ya uchaguzi.
Kimsingi taratibu zote za kuitisha uchaguzi kwa mujibu wa katiba yetu zimezingatiwa na zimekamilika.

Aidha BFT inatoa tamko kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu kufika katika 
uchaguzi uchaguzi, ili kupata viongozi halali kwa mujibu wa katiba, 
waendelee na shughuri za kuendeleza mchezo wa ndondi na kuaandaa timu 
ya taifa kushiriki katika mashindano ya Afrika nchini Mauritius Sept. 2013

BFT inatoa wito kwa watu wote wenye sifa, nia, moyo na uwezo wa kuongoza wajitokeze kuchukua fomu za kugombea uongozi kwani wakati ndio huu. 

*KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA


 Mbunge wa Jimbo la Ilala, jijini Dar es Salaam, na mmoja wa Wenyeviti 
wa Bunge, Mussa Zungu Azzan akiongoza kikao cha Bunge
 Mbunge wa Viti Maalum (CCM) kutoka Mkoani Arusha, Catherine 
Magige akiwa Bungeni mjini Dodoma Juni 26,2013.
 Mbunge wa Nzega, Dk. Hamisi Kingwangalla (kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa CCM nchi za SADC, Kelvin Nyamori (katikati) na Mbunge 
wa Kisesa, Luhanga Mpina, nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma jana.
 Mbunge wa Viti Maalu, Faida Mohamed Bakar akizungumza jambo na 
Mbunge wa Tandahimba, Juma Njwayo nje ya ukumbi wa Bunge mjini 
Dodoma jana.
Mbunge wa Viti Maalum, Faida Mohamed Bakar akifurahia jambo na 
Wabunge wenzake  Juma Njwayo wa Jimbo la Tandahimba, na Dk. 
Hamisi Kingwangala wa Nzega(kushoto) nje ya ukumbi wa Bunge 
mjini Dodoma jana.
 Wapigapicha za Habari wakiwa kazini Bungeni
 Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe akisalimiana na Mbunge wa 
Viti Maalum, Josephine Gezabuke (kulia) nje ya Ukumbi wa Bunge 
mjini Dodoma jana. Kushoto ni Waziri wa Makamu wa Rais, Mazingira,
 Dk. Terezya Huvisa.
 Wabunge wakitoka Bungeni jana

*MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGA MAFUNZO YA UOFISA NA UKAGUZI MSAIDIZI WA CHUO CHA POLISI DAR LEO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimvisha Cheo cha Heshima, Mhitimu wa Mafunzo ya Uofisa na Ukaguzi Msaidizi wa Chuo cha Polisi cha Dar es Salaam, Inspekta John Makuri Imori, wakati wa hafla ya kufunga mafunzo hayo iliyofanyika leo chuoni hapo jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimvisha Cheo cha Heshima, Mhitimu wa Mafunzo ya Uofisa na Ukaguzi Msaidizi wa Chuo cha Polisi cha Dar es Salaam, Inspekta Leah Nicholaus Ncheyeki, wakati wa hafla ya kufunga mafunzo hayo iliyofanyika leo chuoni hapo jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti Cheo cha Heshima, Mhitimu wa Mafunzo ya Uofisa na Ukaguzi Msaidizi wa Chuo cha Polisi cha Dar es Salaam, Akama Mohamed Shaaban, wakati wa hafla ya kufunga mafunzo hayo iliyofanyika leo chuoni hapo jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimvisha Cheo cha Heshima, Mhitimu wa Mafunzo ya Uofisa na Ukaguzi Msaidizi wa Chuo cha Polisi cha Dar es Salaam, Inspekta Alekunda John Urio, wakati wa hafla ya kufunga mafunzo hayo iliyofanyika leo chuoni hapo jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimvisha Cheo cha Heshima, Mhitimu wa Mafunzo ya Uofisa na Ukaguzi Msaidizi wa Chuo cha Polisi cha Dar es Salaam, S/SGT Juma Sadiki Bahati, wakati wa hafla ya kufunga mafunzo hayo iliyofanyika leo chuoni hapo jijini Dar es Salaam.
 Sehemu ya askari waliohudhuria hafla hiyo.

 Aaskari wahitimu wa mafunzo hayo akiwamo na Mwanadada, wakionyesha mchezo wa kujihami na adui wakati wa hafla ya kufunga mafunzo hayo. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPO CHINI

Tuesday, June 25, 2013

*RAIS WA TFF LEODGER TENGA WATAKA MAKOCHA WALIOMALIZA KOZI KUIBUA VIPAJI VYA SOKA NCHINI


Mhitimu wa kozi ya ukocha wa mpira wa miguu kwa ngazi ya pili, Seleman Matola akipongezwa na Rais wa Shirikisho la Soka nchini, Leodgar Tenga kwenye sherehe zilizofanyika jana Uwanja wa Taifa.Kulia ni Mwenyekiti wa DRFA Almas Kassongo na (kushoto) Mkurungenzi wa Ufundi TFF, Sunday Kayuni.
***********************************
RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodger Tenga, amewataka makocha kuhakikisha wanaibua vipaji vya watoto ili kuwa na vipaji vingi baadaye.
Tenga alikuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa kozi hiyo ya ngazi ya pili  iliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kozi hiyo iliyoendeshwa na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa Dar es Salaam (DRFA), ilianza Juni 3 huku ikishirikisha zaidi ya makocha 58.
Tenga alisema Bara la Afrika ndilo bara lenye upungufu mkubwa wa wachezaji watoto, tofauti na mabara mengine, kitu ambacho kinarudisha nyuma maendeleo ya soka.
“Hili ndilo bara ambalo lipo nyuma katika kuibua vipaji, mfano nchi ya Ujerumani pekee ina watoto zaidi ya milioni  moja ambao wanaandaliwa, lakini hapa sijui kama wanafika hata idadi hiyo, hivyo kuna changamoto kubwa katika hilo,” alisema.
Aliwataka kuhakikisha wanayatumia mafunzo hayo katika kuleta mabadiliko katika soka hapa nchini, ambapo pia aliwapongeza kwa kushiriki katika kozi hiyo.
Naye Mwenyekiti wa DRFA, Almas Kassongo amesema kozi hiyo itakuwa mkombozi wa makocha kusaidia timu zao kufanya vizuri na kuendeleza mchezo huo nchini.
"Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Rais wa TFF kwa kukubali kuwa nasi licha ya majukumu mengi aliyonayo, lakini niseme tu kwamba kozi hii imekuwa ya mafanikio kutokana na kushirikisha wachezaji wengi wa zamani," alisema.
Baadhi ya washiriki waliohitimu kozi hiyo ni pamoja na Moses Mkandawile, Shedrack Nsajigwa, Ibrahim Masoud Maestro, Shaffih Dauda, Rahel Pallangyo, Ally Yusuph Tigana, Emanuel Gabriel, Jemedari Said, Benard Mwalala, Edibily Lunyamila, Seleman Matola na wengineo

*TANZANIA YASHINDA TUZO 3 ZA UTUMISHI WA UMMA BARANI AFRIKA NCHINI GHANA.


 By Pascal Mayalla  
Tanzania imeshinda tuzo tatu za juu za ubunifu katika Utumishi wa Umma, barani Afrika, kufuatia Tasisi tatu za Tanzania, kushinda nafasi ya kwanza, na kukabidhiwa vikombe vya ushindi na rais wa Ghana, wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Utumishi wa Umma barani Afrika, yaliyofanyika jana mjini Accra nchini Ghana.

Taasisi za Tanzania zilizoshinda ni Ofisi ya  Ukaguzi ya Taifa, (NAO), Wakala wa Vipimo, (WMA),  na Wakala wa Vitambulisho vya Taifa, (NIDA) kufuatia kufanya vizuri katika maonyesho ya  siku 7 ya shughuli mbalimbali za utumishi wa umma yaliyofikia kilele tarehe 23/06/2013.

Akiuzungumzia ushindi huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Mhe. Celina Kombani, amezipongeza taasisi hizo, zilizolitea sifa taifa hili na kuelezea kufarijika kwake na ushiriki wa  mkubwa wa Tasisi za Tanzania katika maonyesho hayo ambapo jumla ya taasisi 42 kutoka Tanzania, zilishiri.

Akisoma hotuba katika kilele cha maandimisho hayo, Mhe. Kombani ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mawaziri wa Utumishi Barani Afrika, amewataka watumishi wa umma kote barani Afrika, kuwatumikia wananchi kwa  bidii,
unyenyekevu, uadilifu wa hali ya juu, na kueleza utumishi wa umma ni kuwatumikia watu.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Gearge Yambesi, amekiri kuwa Tanzania ni moja ya nchi zinazofanya vizuri sana katika utumishi wa umma barani Afrika, hali inayofanya Tanzania kujijengea heshima kubwa barani Afrika na Ulimwenguni kwa ujumla.

Wakizungumzia kuhusu ushiriki wa Tanzania katika maonyesho hayo, Waziri , Mhe. Celina Kombani,  na Katibu Mkuu, Bwana. George Yambesi, wanaeleza zaidi.


Akizungumzia maonyesho hayo, Mkurugenzi wa Kampuni ya Press and Public Relations (PPR), Bw. Pascal Mayualla, amesema mfulululizo wa vipindi vya redio na Televisheni, kuhusu ushiriki wa Tanzania, katika Maonyesho ya Utumishi wa Umma barani Afrika, vitaanza kuonekane kesho, katika vituo mbalimbali vya redio na Televisheni.

*WANAWAKE WANA UWEZO WA KUBADILISHA MAISHA YA MTANZANIA


Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa Kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa akitoa hotuba yake  wakati wa ufunguzi  wa mafunzo ya siku tatu ya wanawake wajasiriamali yanayoendelea kwenye  ukumbi wa Bwalo la Maafisa la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT),Mgulani jijini Dar es salaam.
***************************************
NA BELINDA KWEKA – MAELEZO
WANAWAKE wakiwezeshwa kiuchumi na kupatiwa elimu ya msingi ya ujasiriamali, kuepuka maradhi hatarishi na kufahamu haki zao katika jamii, umasikini utapungua,  kipato  kitaongezeka na maisha ya Watanzania yatabadilika. 
 Hayo  yalisemwa leo na Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa Kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa wakati wa ufunguzi  wa mafunzo ya siku tatu ya  wanawake wajasiriamali yanayoendelea kwenye  ukumbi wa Bwalo la Maafisa la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT),Mgulani jijini Dar es salaam.

Mama Anna Mkapa ambaye pia ni Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa   alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wa kiuchumi na kijamii  wajasiriamali  hao kutoka mikoa yote Tanzania Bara na Visiwani, ambapo jumla ya wanawake wapatao 264 wanashiriki.

“Mfuko wa Fursa Sawa Kwa Wote umekusudia kwa nguvu zake zote kuendeleza vita ya hii ya kuwawezesha wanawake  nchini  kujikwamua katika wimbi la umasikini, maradhi na ujinga,” alisisitiza Mama Mkapa.
 Aidha ameiomba Serikali, Asasi za kiraia, taasisi za dini, wahisani binfasi ndani na nje ya nchi, kusaidia  wanawke haswa wa vijijini   kujikwamua na umasikini. 

 Mama Mkapa  aliongeza  kuwa mfuko huo, kwa kipindi cha miaka 16  zaidi ya wanawake 6,820 wamepata mafunzo ya stadi za biashara na wengine  4,500 wamepata fursa ya kushiriki maonyesho mbalimbali ya ndani na nje ya nchi kwa kupitia EOTF ili  kutangaza na kuuza bidhaa zao.

 Naye Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko Dk. Abdallah Kigoda  akifungua mafunzo hayo alisema  Serikali imeanzisha utaratibu wa kuweka kumbukumbu za mkopo katika mabenki kwa kupitia ‘Credit Reference Bureau’ ili kuweza kusaidia kuwafahamu wateja, na kuwaasa wajasiriamali wanapokopa wakumbuke kulipa kwani uaminifu ni kitu muhimu katika biashara.
“Suala lingine la kulipa kipaumbele ni lile la kuongeza thamani ya mazao wanayoyazalisha na tuache kuwazalishia watu wengine bidhaa wakaenda  kuongezea thamani kidogo tu kama vile kwa kufunga na kuweka nembo ya kibiashara na kuuza kwa bei kubwa,” alisema Dk. Kigoda. 
Aliahidi kuwa Wizara yake iko makini kufanya linalowezekana kushirikiana na wajasiliamali hao kutatua  tatizo hilo la kuuza malighafi badala ya bidhaa iliyoongezwa thamani  ili kuongeza ajira na kupunguza umasikini.

*WANAFUNZI WALIOSOMA SHULE ZA KATA VYUO VIKUU WAMTAKA LOWASSA AWANIE URAIS 2015



Mbunge wa Monduli, ambaye pia ni waziri mkuu mstaafu, Edward Lowasa, akisalimiana na wanafunzi wa chuo kikuu cha UDOM waliotoka shule za sekondari za kata, wakati walipofika nyumbani kwake mkoani Dodoma kutoa shukrani zao kwa hatua waliyofikia kielimu.


Hamida Salum mwanafunzi wa mwaka wa kwanza UDOM, akizungumza kwenye hafla hiyo Juni 25, 2013

 
Mh. Lowasa katikati, Dkt. Mahanga (Kulia) na Parseko Korne wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi hao.KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPO CHIN

*MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA 24 WA MWAKA WA TUME YA NGUVU ZA ATOMIKI TANZANIA


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia washiriki wa kutano, wakati akifungua rasmi Mkutano wa 24 wa mwaka wa nguvu za Atomiki Tanzania, wa Utafiti na Mfunzo ya ukuaji wa Teknolojia ya Sayansi ya Nyuklia, ulioanza leo katika Ukumbi wa AICC jijini Arusha.
 Baadhi ya washiriki wa Mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo leo, katika Ukumbi wa AICC jijini Arusha.
 Baadhi ya washiriki wa Mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo leo, katika Ukumbi wa AICC jijini Arusha.
 Picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mkutano huo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Ofisa Utafiti wa Mitambo ya Nyuklia, Kitengo cha Matengenezo, Yesaya Sungita, wakati Makamu alipotembelea Taasisi ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania, iliyopo eneo la Njiro jijini Arusha leo, Juni 25, 2013 baada ya kufungua mkutano wa 24 wa mwaka wa nguvu za Atomiki Tanzania, wa Utafiti na Mfunzo ya ukuaji wa Teknolojia ya Sayansi ya Nyuklia, ulioanza leo katika Ukumbi wa AICC jijini Arusha.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa msimamizi wa Mashine ya kutafiti Vyakula na Mazingira, Remigius Kawala, wakati Makamu alipotembelea Taasisi ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania, iliyopo eneo la Njiro jijini Arusha leo, Juni 25, 2013 baada ya kufungua mkutano wa 24 wa mwaka wa nguvu za Atomiki Tanzania, wa Utafiti na Mfunzo ya ukuaji wa Teknolojia ya Sayansi ya Nyuklia, ulioanza leo katika Ukumbi wa AICC jijini Arusha.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia na kusikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Kinga ya Mionzi, Ukaguzi wa  Vifaa, Dkt. Willbrod Muhogola, wakati Makamu alipotembelea Taasisi ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania, iliyopo eneo la Njiro jijini Arusha leo, baada ya kufungua mkutano wa 24 wa mwaka wa nguvu za Atomiki Tanzania, wa Utafiti na Mfunzo ya ukuaji wa Teknolojia ya Sayansi ya Nyuklia, ulioanza leo katika Ukumbi wa AICC jijini Arusha. 
 Baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ta Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania, iliyopo eneo la Njiro jijini Arusha, wakimsikiliza Mhe. Makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akizungumza nao.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania, iliyopo eneo la Njiro jijini Arusha, baada ya kuzungumza nao alipotembelea Taasisi hiyo leo

*WANASWA KWENYE BODABODA WAKIWA NA BASTOLA YENYE RISASI NJE YA BENKI YA POSTA DAR


 Askari kanzu (kulia) akiwa ameshika bastola aliyokutwa nayo mtu mmoja aliyekuwa amepakiwa katika pikipiki aina ya Boxer yenye namba za usaji T 961 CJW katika mtaa wa Makunganya jirani kabisa na benki ya Posta jijini Dar es Salaam leo mchana. Kutokana na kuongezeka kwa matukio ya ujambazi wa kutumia pikipiki na silaha, polisi wameimarisha ulinzi na hasa katika maeneo ya mabenki, ambapo leo wamebahatika kucheza karata yao ya kwanza na kuwanasa jama hao. Haikuweza kufahamika mara moja kuwa jamaa hao waliokutwa na silaha hiyo kuwa walikuwa wakiimiliki kihalali ama la, na sababu za kuwa eneo hilo mida hiyo ya mchana wakiwa na silaha hiyo.
 Watuhumiwa hao wakijaribu kuwasiliana na ndugu jamaa zao kutafita msaada, baada ya kunaswa.
Askari Kanzu, akiikagua silaha hiyo na kukuta ikiwa na risasi za kutosha......Picha kwa hisani ya Habari Mseto Blog

*MICHAEL JACKSON AIBUKIA BONANZA LA TBL'S FAMILY DAY JIJI DAR

 WMsanii wa kikundi cha  sanaa cha Afrigay Talent Base cha Magomeni Dar es Salaam, Michael Jackson wa Tanzania, akiwaongoza wenzake kutoa burudani wakati wa hafla ya wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), pamoja na familia zao Kunduchi Water Park, Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Fedha wa TBL, Kelvin (kulia), akimkabidhi George Magombeka zawadi ya saa ya ukutani baada ya kuwa mshindi wa riadha katika bonanza hilo la kukata na shoka lililofanyika Kunduchi, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Meneja Uhusiano Mambo ya Nje wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Emma Oriyo (kulia) akimkabidhi zawadi  .Mbwana Milanzi baada ya kuwa mshindi wa kwanza wa mbio za magunia katika hafla ya Siku ya wafanyakazi wa TBL kufurahi na familia zao kwenye ufukwe wa Bahari ya Hindi, Kunduchi Dar es Salaam
 Meneja Uhusiano Mambo ya Nje wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Emma Oriyo  akimkabidhi zawadi  .mmoja wa washindi wa riadha kwa upande wa wananwake. Kulia ni Mhandisi Ujenzi wa TBL, John Malisa.
 Wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), wakifurahi na familia zao kwa kucheza kushindana kuvuta kamba katika ufukwe wa Bahari ya Hindi, Kunduchi Dar es Salaam, wakati wa sherehe 'Tbl's Family Day'.