Thursday, June 20, 2013

*MBOWE, LEMA WAJISALIMISHA KITUO CHA POLISI ARUSHA


Freeman Mbowe (kulia) na Godbless Lema.
**********************************************************
Na Veronica Mheta, Arusha
Mbunge wa jimbo la Arusha Godbless Lema na mwenyekiti wa chama chademokrasia na maendeleo na kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni Freeman Mbowe wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani hapa ilikuweza kutoa ushahidi wa tukio la bomu lililotokea kwenye mkutano wa kampeni wa chama hicho.
Viongozi hao wanashikiliwa baada ya mwenyekiti huyo kudai anawajuwa waliolipua bomu na wanao mkanda wa tukio zima la ulipuaji huo kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani ulikuwa ufanyike 16 mwezi huu jijini hapa.
Akizungumza na wanahabari kwenye ofisi za makao makuu ya jeshi la polisi mkoani hapa jana kamishna wa upelelezi wa jeshi hilo Charles Chagonja alisema kuwa jeshi hilo linawataka viongozi hao waweze kuwasilisha ushahidi huo na kuwa kama hawatakubali kwa hiyari basi litawatafuta popote walipo.
Kamishna Chagonja alisema kuwa ushahidi wa tukio hilo ni muhimu kwa amani ya nchi yetu na kuwa machafuko yanayotokea kwenye jiji hili hayakubaliki kwani nchi yeyote iliyoingia kwenye machafuko ilichangiwa na vyombo vya habari kuripoti kwa ushabiki badala ya kutumia taaluma.
“Matukio ya ulipuaji wa mabomu kwenye nchi yetu hayakubaliki na kuwa mtu mwenye ushahidi wa tukio la bomu kwenye mkutano wa chadema atusaidie kuweza kufanya upelelezi wa tukio hili nawaombeni wanahabari kuacha ushabiki na kujikita katika taaluma yenu”alisema Chagonja.
Wakati huo huo Maiti ya aliekuwa katibu wa kata ya Sokon 1 wa chama hicho Judith William Mushi imepelekwa kuzikwa kwenye kata hiyo kwa heshima zote za chama hicho wakiwemo wabunge mbali mbali  wa chama hicho waliopo mkoani hapa baada ya mwenyekiti wao kuwataka kushiriki kwenye tukio hilo.
Baadhi ya wabunge wa chama hicho waliopo mkoani hapa wameshiriki msiba huo ni pamoja na mch.Peter Msigwa,Joseph Mbilinyi,Theresia Pareso,Ezekie Wenje,John Mnyika,na viongozi mbali mbali wa chama hicho kutoka makao makuu na mikoa ya jirani.
Aidha baadhi ya wananchi waliongea na mwanahabari hii waliieleza kuwa tumekuwa tukitafuta vipaji vya riadha hapa nchini lakini kumbe wapo hadi wabunge wanaoweza kutuwakilisha vizuri nchi yetu na tukapata hadi medali akiwemo mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema.
“unajua ndugu mwandishi mabomu sio mchezo yalimfanya mbunge kutimua mbio hadi maeneo ya sanawari hapa vipaji vipo ila hatujaweka mkazo kwenye kutafuta vipaji “alisema Yusuph
Msafara wa kuupeleka mwili wa katibu wa kata ya Sokon 1 ulipitia kwenye barabara za Sokoine kuelekea Esso hadi Pallotkwenye nyumba yake ya milele na kuhudhuriwa na wafuasi wa chama hicho wengi wakitembea kwa miguu umbali wa kilometa sita kuoka Hospital ya mkoa ya Mout Meru.

No comments:

Post a Comment