Benki ya NMB imefadhili michezo ya UMITASHUMTA katika Manispaa ya Sumbawanga kwa kutoa vifaa vya michezo vyenye thamani ya shilingi milioni 9. Lengo kuu la ufadhili huo ni kusaidiana na UMITASHUMTA katika kuibua na kuendeleza vipaji vya michezo kwa shule za msingi nchini Tanzania.
Meneja wa NMB Tawi la Sumbawanga, John Chinguku (kuli) akimkabidhi Afisa Elimu, Modesta Zambi, sehemu ya vifaa vya michezo vitakavyotumika kwenye michezo ya UMITASHUMTA katika Manispaa ya Sumbawanga. Makabidhiano hayo yalifanyika hivi karibuni kwenye manispaa hiyo.
Maofisa wa Benki ya NMB na maofisa wa Manispaa ya Sumbawanga wakisikiliza maelekezo kutoka kwa Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Sumbawanga, John Chinguku (tatu kulia) wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa hivyo vya michezo.
Sehemu ya mipira iliyotolewa na Benki ya NMB kwa ajili ya UMITASHUMTA.
No comments:
Post a Comment