Waahadhiri wa Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) wakiimba wimbo wa Solidarity, kumaanisha mshikamano katika madai yao.
Kaimu Mwenyekiti wa TEKUASA, Amani Simbeye, akifungua mkutano kati ya waandishi wa Habari na Waahadhiri wa Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU).
Waahadhiri wa Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU) wakifuatilia kwa umakini kikao hicho wakati kikiendelea.
Mmoja wa Waahadhiri wa Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU) , akikazia jambo ya yale ambayo yalikuwa yamezungumzwa.
Mmoja wa Waahadhiri wa Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU), akitila mkazo na kujibu swali ambalo liliulizwa na mmoja wa waandishi wa Habari.
Waahadhiri wa Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) wakigonga meza kuashiria kuunga MKONO Hoja zilizo somwa.
***********************************
HALI si Shwari Ndani ya Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) baada ya Uongozi wa Chama cha Wahadhili wa Chuo hicho (TEKUASA) na wanachama wake kutangaza mgomo wa kutotunga mitihani ya kufungia Mhula, Mitihani ambayo inatarajiwa kufanyika Julai Mosi Mwaka huu kwa kile walichodai Menejimenti ya Chuo kutotoa majibu ya matatizo yao.
Mgomo huo umetangazwa leo na Kaimu Mwenyekiti wa Tekuasa Amani Simbeye katika Mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Chuo hicho kilichopo Block T kata ya Iyela Jiji na Mkoa wa Mbeya na kuhudhuriwa na zaidi ya Wahadhili 30.
Simbeye amesema kuna mambo mengi na changamoto za elimu inayotolewa Chuoni hapo ambazo Menejimenti ya Chuo inahusika moja kwa moja hivyo kuhatarisha mustakabali wa Elimu Nchini hususani inayotolewa Chuoni hapo ambapo ameongeza kuwa zaidi ya yote ni kukosa ushirikishwaji wa maamuzi yanayohusu Taaluma.
Kwa taarifa zaidi na madai ya Wahadhili hao hadi kupelekea kususia kutunga mitihani ya kumaliza muhula inatarajiwa kufanyika Julai Mosi Mwaka huu yameandikwa kwenye barua hapo chini lakini habari kamili itawajia baadaye kwa Lugha ya Kiswahili endelea kuwa nasi.
No comments:
Post a Comment