Sadifa ameyasema hayo wakati akizungumza na wanachama wasomi wa UVCCM kutoka katika vyuo vikuu mkoani kilimanjaro katika hafla ya kuwaaga wasomi hao na ambapo pia ametunuku vyeti vya uanachama kwa wanafunzi 312 pamoja na kuwakabidhi kadi za uanachama wanachama wapya.
Amesema bila amani na muungano wa wananchi maendeleo hayawezi kupatikana katika nchi ambpo aliwataka vijana kuwa mtari wa mbele kuwaelimisha wananchi wa kawaida juu ya umuhimu wa kuenzi, kudumisha na kuimarisha muungano wa zanzibar na Tanganyika kama njia pekee ya kuhakikisha nchi inakuwa na amani siku zote.
Katibu wa UVCCM manispaa ya Moshi, Bwana Makwaiya akisakata Rumba muda mfupi baada ya maandamano kuwasili katika makao makuu ya CCM mkoa wa kilimanjaro |
“Vijana tuna wajibu kubwa wa kuwaenzi waliotuletea muungano wetu wa sasa, taaluma zetu ziwe dira ya jamii katika kuenzi, kudumisha na kuimarisha muungano wetu kwani ndio njia pekee ya kusaidia kudumisha amani na usalama wan chi yetu, tuepuke kujiingiza katika mkumbo wa wale wanaodai nchi haitatawalika,” amesema
Hata hivyo Sadifa amewataka vijana kutodanganyika na vyama vinavyoeneza chuki na maandamano yasiyokuwa na msingi wowote huku akifafanua kuwa kisheria kuandamana na haki ya msingi lakini ifuate sheria na yassingilie haki za wengine.
Sadifa akikabidhi cheti cha unachama kwa mwanafunzi wa chuo kikuu muccobs jana, jumla ya wanavyuo 312 walipata vyeti vya uanachama wa UVCCM. |
“Chama pekee katika nchi hii ni CCM, kuna vyama vingine vimeanzishwa ambavyo mimi binafsi naviita ‘Saccos’, hauwezi ukajikopesha fedha kienyejienyeji kama alivyofanya Dk. Slaa! Vijana tuwe makini na saccos hizi ambazo ajenda zao ni kukopeshana na vurugu tu,” amesema Sadifa.
Kwa upande wake mwenyekiti wa shirikisho la wanafunzi wa vyuo vikuu wanachama wa CCM kilimanjaro, Wakati Mtulya akizungumzia changamoto wanazokumbana nazo, alisema kumekuwa na urasimu ndani ya bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, ambapo mikopo imekuwa ikitolewa kwa watu wasiostahili huku walengwa wakiendelea kutaabika.
Sadifa (aliyevaa suti) akiongoza vijana kucheza kwaito katika ukumbi wa CCM mkoa wa Kilimanjaro |
“Mikopo ni yetu, sio ruzuku, lazima tukopeshwe kwa wakati kwani lazima tutairudisha lakini jambo la kusikitisha, bodi hii imekuwa ikitoa mikopo kwa watoto wa masaki, huku sisi watoto wea mkulima tukiendelea kuzungushwa na kuwekewa masharti magumu ili kupata mikopo hiyo, hili ni tatizo,” amesema Mtulya (habari na TAIFA LETU.com).
No comments:
Post a Comment