Wednesday, June 19, 2013

*MAADHIMISHO YA SIKU YA UGONJWA WA SIKOSELI DUNIANI, YAFANYIKA JIJINI DAR LEO


 Mwenyekiti wa Mfuko wa Sikoseli Tanzania, Grace Rubambey (katikati) akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya ugonjwa wa  Sikoseli Duniani jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Mfuko huo, Dk Julie Makani,  Balozi wa Canada nchini, Alexandre Leveque na mmoja wa watu wanoishi na ugonjwa huo, Arafa Salim Said.
  Balozi wa Canada nchini, Alexandre Leveque (katikati) akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya ugonjwa wa Sikoseli Duniani jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Mfuko wa Sikoseli Tanzania Dk Julie Makani na Mwenyekiti wa mfuko huo, Grace Rubambey na mmoja wa watu wanoishi na ugonjwa huo, Arafa Salim Said.
  Makamu Mwenyekiti wa Mfuko wa Sikoseli Tanzania, Dk Julie Makani (kushoto) akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya ugonjwa wa Sikoseli Duniani jijini Dar es Salaam leo. Tanzania ni nchi ya nne duniani kwa kuwa na idadi kubwa ya watu wanaougua ugonjwa wa sikoseli.
   Meneja wa Benki ya KCB Tawi la Msimbazi, Philipo Pilla (kulia) akizungumza wakati wa maadhjimisho hayo. Benki ya KCB ni mmoja wa wadhamini wa Mfuko wa Sikoseli Tanzania.
 Mratibu wa Huduma za Ugonjwa wa sikoseli katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Dk. Deogratias Soka (kulia) akizungumza kuhusu hali ya ugonjwa huo katika hospitali hiyo katika maadhimisho hayo. Inakadiriwa kuwa katika ya watoto 8,000 hadi 10,000 kuzaliwa na ugonjwa huo nchini Tanzania kila mwaka.
Baadhi wa watu walioshiriki maadhimisho jijini Dar es Salaam leo. Ugonjwa wa sikoseli ni ugonjwa wa kurithi unaosababisha mabadiliko yasiyo ya kawaida katika chembechembe nyekundu za damu hivyo mtu hawezi kuambukizwa kwa njia yoyote ile kama vile kuishi au kuwa karibu na mgonjwa wa sikoseli.

No comments:

Post a Comment