Tuesday, June 25, 2013

*KAMATI YA MAANDALIZI YAFANYA KIKAO NA UBALOZI, WASHINGTON, DC


Afisa Ubalozi Suleiman Saleh (kushoto) akisalimiana na Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV Bwn. Idd Sandaly wakati akiwakaribisha kamati ya maandalizi ya sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo na Tamasha la utamaduni wa kiswahili Marekani Ubalozini kwenye kikao cha maandalizi ya mwisho mwisho ya sherehe ya Vijimambo pamoja na mambo mengi yaliyojadiliwa, ulinzi na kuhofiwa watu kuwa wengi ndiyo maswala yaliyochukua muda mrefu kuyajadili na kushauriwa watu kuwahi mapema na kwa sababu kutakua na zoezi la kukaguliwa kabla ya kuingia ukumbini na nafasi za kukaa kwenye ukumbi ni watu 500 kwa kuepuka usumbufu wa msururu mrefu jaribu kufika mapema milango itakua wazi kuanzia saa 3 asubuhi.
Mwenyekiti wa kamati Bwn. Baraka Daudi akitia saini kitabu cha wageni.
Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV Bwn Idd Sandaly akitia saini kitabu cha wageni.
Katibu msaidizi wa kamati Julius Katanga akitia saini kitabu cha wageni.
Kaimu Balozi Mama Lily Munanka (kati) akiongoza kikao cha kamati ya maandalizi kilichofanyika Ubalozi wa Tanzania Washington, DC Jumatatu June 24, 2013 wengine katika picha kutoka kushoto ni Bwn. Idd Sandaly, Bwn. Baraka Daudi, Afisa Ubalozi Suleiman Saleh na Dj Luke.
Kutoka kushoto ni Afisa Ubalozi Edward Masanja, Idd Sandaly, Baraka Daudi, Kaimu Balozi Mama Lily Munanka, Afisa Ubalozi Suleiman Saleh Dj Luke na Julius Katanga.
Kamati na maofisa Ubalozi wakimsubili Kaimu Balozi mama Lily Munanka (hayupo pichani).
Bwn. Idd Sandaly, Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV(kushoto) wakiwa kwenye kikao cha kamati ya maandalizi na maafisa Ubalozi wakiongozwa na kaimu Balozi mama Lily Munanka katika kujadili maandalizi ya miaka 3 ya sherehe ya Vijimambo na Tamasha la Utamaduni wa Kiswahili.
Afisa Habari wa Ubalozi Mindi Kasiga akichangia jambo.

No comments:

Post a Comment