Tuesday, June 25, 2013

*RAIS WA TFF LEODGER TENGA WATAKA MAKOCHA WALIOMALIZA KOZI KUIBUA VIPAJI VYA SOKA NCHINI


Mhitimu wa kozi ya ukocha wa mpira wa miguu kwa ngazi ya pili, Seleman Matola akipongezwa na Rais wa Shirikisho la Soka nchini, Leodgar Tenga kwenye sherehe zilizofanyika jana Uwanja wa Taifa.Kulia ni Mwenyekiti wa DRFA Almas Kassongo na (kushoto) Mkurungenzi wa Ufundi TFF, Sunday Kayuni.
***********************************
RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodger Tenga, amewataka makocha kuhakikisha wanaibua vipaji vya watoto ili kuwa na vipaji vingi baadaye.
Tenga alikuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa kozi hiyo ya ngazi ya pili  iliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kozi hiyo iliyoendeshwa na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa Dar es Salaam (DRFA), ilianza Juni 3 huku ikishirikisha zaidi ya makocha 58.
Tenga alisema Bara la Afrika ndilo bara lenye upungufu mkubwa wa wachezaji watoto, tofauti na mabara mengine, kitu ambacho kinarudisha nyuma maendeleo ya soka.
“Hili ndilo bara ambalo lipo nyuma katika kuibua vipaji, mfano nchi ya Ujerumani pekee ina watoto zaidi ya milioni  moja ambao wanaandaliwa, lakini hapa sijui kama wanafika hata idadi hiyo, hivyo kuna changamoto kubwa katika hilo,” alisema.
Aliwataka kuhakikisha wanayatumia mafunzo hayo katika kuleta mabadiliko katika soka hapa nchini, ambapo pia aliwapongeza kwa kushiriki katika kozi hiyo.
Naye Mwenyekiti wa DRFA, Almas Kassongo amesema kozi hiyo itakuwa mkombozi wa makocha kusaidia timu zao kufanya vizuri na kuendeleza mchezo huo nchini.
"Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Rais wa TFF kwa kukubali kuwa nasi licha ya majukumu mengi aliyonayo, lakini niseme tu kwamba kozi hii imekuwa ya mafanikio kutokana na kushirikisha wachezaji wengi wa zamani," alisema.
Baadhi ya washiriki waliohitimu kozi hiyo ni pamoja na Moses Mkandawile, Shedrack Nsajigwa, Ibrahim Masoud Maestro, Shaffih Dauda, Rahel Pallangyo, Ally Yusuph Tigana, Emanuel Gabriel, Jemedari Said, Benard Mwalala, Edibily Lunyamila, Seleman Matola na wengineo

No comments:

Post a Comment