Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kupokea msaada wa hundi ya milioni kumi kutoka Zantel kwa ajili ya Chama cha Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT) leo jijini Dar es Salaaam, kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu Zantel Bw. Pratap Ghose.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akipokea hundi ya shilingi milioni kumi kwa ajili ya Chama cha Ngumi za Ridhaa Tanzania, kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu Zantel Bw. Pratap Ghose, wapili kushoto ni Rais wa Chama cha Ngumi Tanzania Bw. Mutta Rwakatare na wapili kulia ni Katibu Chama cha Ngumi Tanzania Bw. Makole Mashaga.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (kulia), Afisa Mtendaji Mkuu Zantel Bw. Pratap Ghose (kushoto) pamoja na viongozi kutoka Chama cha Ngumi Tanzania (BFT) wakiunganisha mikono kwa pamoja kuonyesha ushirikiano wakati wa makabidhiano ya hundi ya shilingi Milioni kumi kama msaada kutoka Zantel kwa Chama cha Ngumi Tanzania (BFT).
Rais wa Chama cha Ngumi Tanzania Bw. Mutta Rwakatare akitoa shukrani kwa Zantel baada ya kukabidhiwa hundi ya shilingi milioni kumi kuinua mchezo wa ngumi, kushoto ni Katibu Chama cha Ngumi Tanzania Bw. Makole Mashaga na kulia ni Mjumbe wa Maendeleo ya Wanawake Bi. Aisha George Voniatis.
Picha na Genofeva Matemu
Na: Genofeva Matemu –
Afisa Mawasiliano Serikalini (WHVUM)
Wadau mbalimbali wa
michezo nchini wameshauriwa kuwekeza katika vyama vya michezo ili kuinua
michezo nchini na kuweza kuleta maendeleo ya kweli katika sekta ya Michezo.
Kauli hiyo imetolea
na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara alipokuwa
akipokea msaada wa hundi ya milioni kumi kutoka Zantel kwa ajili ya Chama cha
Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT) leo jijini Dar es Salaaam.
Dkt. Mukangara amesema
kuwa sekta ya michezo inahitaji uwekezaji mkubwa hivyo serikali haiwezi
kutegemewa katika kufanikisha maendeleo ya michezo bali kuwekeza katika kampuni
nyingine kama ilivyo kwa Zantel.
“Kwa hakika Michezo
ni sekta inayohitaji uwekezaji mkubwa kama ilivyo katika sekta nyingine yoyote
ile ya maendeleo. Bila kuwekeza ipasavyo hatuwezi hata kidogo kupata maendeleo
tunayoyatamani kama ilivyo kwa wenzetu waliopiga hatua kubwa katika Michezo duniani”
amesema Dkt Mukangara.
Katika kuonyesha kuwa
michezo ni afya Dkt. Mukangara alifafanua kuwa umuhimu wa kuwekeza katika
Michezo siyo tu katika kushinda mashindano ya kimataifa ua ya ndani bali pia
upo katika kutayarisha wachezaji wa kutoka ngazi mbalimbali na kuhakikisha kuwa
afya za watu zinakuwa imara na hivyo kuwa na uwezo mkubwa wa kulitumikia taifa
lao.
Aidha Katibu Mtendaji
Baraza la Michezo Tanzania BW. Henry Rihaya amewataka viongozi wa michezo kuwa
na maadili mazuri na kusimamia matumizi mazuri ya fedha wanazopata ili
kuiwezesha serikali kuwa nao bega kwa bega katika kuleta maendeleo ya michezo
nchini.
Naye Rais wa Chama
cha Ngumi Tanzania Bw. Mutta Rwakatare amemshukuru Waziri Mukangara pamoja na
Zantel kwa ushirikiano waliouonyesha na kuahidi kuitangaza Boxing nchini na nje
ya nchi huku wakiendelea kuinua vipaji kwa vijana wadogo katika mchezo wa
Boxing.
Zantel imeamua
kudhamini Chama cha Netibali, Chama cha Mchezo wa Ngumi za Ridhaa pamoja na
Chama cha Mchezo wa Karate katika kufanikisha programme walizojiwekea wakiwa na
lengo la kuleta maendeleo ya michezo nchini.
No comments:
Post a Comment