Benki ya NMB imefadhili maonyesho ya ubunifu wa watoto waliokusanywa na Tanzania Mitindo House. Maonyesho ambayo yatahusisha shughuli mbali mbali za kazi za mikono ambazo watoto wenye vipaji wamekua wakizifanya. Maonyesho haya yataanza tarehe 8 Juni hadi tarehe 9 juni 2013 kuanzia saa 9 hadi saa 2 usiku pale Tanzania Mitindo House.
Kwa msaada wa benki ya NMB, watoto hawa watauza kazi zao na kujipatia fedha ambazo zitawekwa moja kwa moja kwenye akaunti zao za NMB. Fedha hizi zitawasaidia watoto hawa katika kuendeleza maisha yao ya kila siku hasa kielimu.
Tanzania Mitindo House ni Taasisi isiyo ya kiserikali ambayo imedhamiria kukusanya na kuendeleza Vipaji vya watoto yatima ambavyo vingedidimia bila msaada wowote. Watoto hawa wanawakaribisha watu wote waweze kutembelea maonyesho ya kazi za mikono yao.
Mtoto Ahmed kutoka shule ya wasiosikia Buguruni kutoka nyumba ya watoto Yatima Tanzania Mitindo House akionyesha ubunifu wa kazi yake wakati wa masomo ya kazi za mikono.
Mtoto Frank kutoka nyumba ya watoto Yatima Tanzania Mitindo House akionyesha umahiri wa kuchanganya rangi katika michoro tofauti tofauti.Frank anauwezo wa kuona lakini hana uwezo wa kusikia vizuri ni mtoto mwenye kipaji ajabu.
No comments:
Post a Comment