Tuesday, June 11, 2013

*KIEMBA AKATA MZIZI WA FITINA, ASAINI SIMBA MKATABA WA MIAKA 2 KWA DAU LA SH. M 50


 Kaka wa mchezaji wa Simba, Amri Kiemba (wa pili kushoto) akisaini kwa niaba ya mdogo wake kuchukua fedha za usajili kwa mkataba wa miaka miwili jumla ya Sh. Milioni 50, baada ya kiungo huyo kukubali kumwaga wino Mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kuichezea Klabu hiyo ya Simba SC wakati wa zoezi hilo lililofanyika leo mchana. Wa pili (kulia) ni Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Joseph Itang'are 'Kinesi' na Damian Manembe (kulia) na Salum Pamba, Wajumbe wa Kamati ya Utendaji. Picha kwa hisani ya Bin Zubeiry
Amri Kiemba Pichani, ambaye alikuwa gumzo kila kukicha hukua akielezewa kuwa tayari alikuwa ameshamwaga wino kwa mahasimu wa Simba Yanga na kupewa mkataba wa miaka miwili na kitita cha Sh. milioni 38, huku akiahidiwa kulipwa mshahara wa Sh. 90,000 kwa mwezi ambao ulikuwa umezidi ule anaopokea kwa wekundu hao. 

Kwa zoezi hilo la kumsainisha Kiungo huyo sasa Klabu ya Simba imekata mzizi wa fitina na kuzima maneno yote yaliyokuwa yameenea mtaani kuwa Kiemba alikuwa katika harakati za kusajiliwa na Yanga.

Lakini pia Inawezekana Wekundu hao wameshtukia dili baada ya kusikia mchezaji huyo amekuwa 'LULU' huko nchini Morocco na kuonekana kuvivutia baadhi ya Vilabu vilivyoonyesha nia ya kumhitaji kiungo huo, hivyo inawezekana Simba wamecheza Karata ya Dume ili kuwahi kitita cha kumuuza Kiungo huyo iwapo waarabu hao watafika bei. ''Kila la kheri Kiemba na huu ndiyo msimu wa mavuno''...

No comments:

Post a Comment