Tuesday, June 4, 2013

MWILI WA MANGWEA WAWASILI WAPOKELEWA KWA MAANDAMANO MAKUBWA


 Maeflu ya mashabiki wa muziki wa kizazi kipya, wakiusindikiza mwili wa marehemu, Albert Mangwea baada ya kuupokea kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere leo mchana.
  Maeflu ya mashabiki wa muziki wa kizazi kipya, wakiusindikiza mwili wa marehemu, Albert Mangwea baada ya kuupokea kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere leo mchana.
 Mashabiki hao wakizuia gari lililobeba mwili wa marehemu ili lishushwe jeneza hilo wabebe wenyewe huku wakiimba.
 P Funku, akishiriki na mashabiki kusukuma gari hilo.....
 Sehemu ya maandamano hayo........
 Maandamano hayo yaliyounganika na pikipiki...
 Wengine walikuwa wakiunga maandamano hayo kwa kukimbia mbio......
******************************

*Matukio na Vituko wakati wa kuwasili mwili wa Ngwair

NA MWANDISHI WETU
MWILI wa marehemu Albert Mangwea 'Ngwear', ambaye ni msanii wa muziki wa kizazi kipya, umewasili nchini leo mchana na kufuatiwa maandamano makubwa, ambayo yaligubikwa na vituko mbalimbali.

Baada ya mwili wa msanii huyo aliyefariki nchini Afrika Kusini Mei 28 mwaka huu kuwasili, watu mbalimbali waliojitokeza kuupokea mwili huo walizunguka gari iliyobeba mwili na kulisukuma gari hilo huku wakilifuata taratibu likitokea Uwanja wa ndege wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, hadi Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Mojawapo ya kituko kilichokea kabla ya mwili huo kutoka eneo la uwanja wa ndege ni kibaka mmoja kujaribu kukwapua simu, lakini watu walijitokeza katika mapokezi hayo ya mwili wa Ngwair, walimnasa na kumpa kipigo cha mbwa mwizi na kisha kumuachia akiwa hajapata madhara makubwa.

Maandamano hayo yaliendelea huku mashabiki wa muziki wa kizazi kipya wakiendelea kuzunguka gari hilo, huku wakiimba nyimbo mbalimbali kama 'kalale pema peponi kamanda Kambanda', 'tutakukumbuka daima milele iko siku mi nawe tutaonana tena mwenzangu'.

Wasanii mbalimbali walikuwepo kwenye maandamano hayo yasiyo rasmi, baadhi ya wasanii hao walikuwa ndani ya magari yao mbele ya gari lililobeba mwili wa marehemu walikuwa ni Chegge, Ally Kiba, Abdu Kiba, huku Mrisho Mpoto, Keisha na mchezji wa zamani wa Coastal Union, Simba na Azam, Uhuru Selemani wakiwa nyuma ya gari la maiti.

Mashabiki waliendelea kuusindikiza mwili wa marehemu hadi maeneo ya Jet, ambapo msanii T.I.D na Prodyuza P. Funky, waliposhuka kwenye magari waliyokuwa wamepanda na kuungana na mashabiki hao na kuwafanya mashabiki kuwashangilia vilivyo, huku wakihamasisha kwa kuimba ''Mshusheni tumbebe mshusheni tumbebe''.....

Wakati maandamano hayo yakiendelea mashabiki hao walianza kuzuia gari na kutaka mwili wa marehemu Albert Mangwea ushushwe, ili waubebe

No comments:

Post a Comment