Wednesday, May 21, 2014

WAZIRI MBARAWA AFUNGUA MAONESHO YA 9 YA ELIMU YA JUU,SAYANSI NA TEKNOLOJIA.


 Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa (katikati) na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Jenista Muhagama, wakimsilikiza Afisa Uhusiano wa Chuo cha Kikristo cha Uganda Prim Tumuramye baada ya ufunguzi wa Maonesho ya 9 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yaliyoanza leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee
 Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Jenista Muhagama, akimueleza jambo Naibu Mkuu wa Chuo cha Ualimu cha Dar es Salaam (DUCE) Profesa Godliving Mtui (katikati) kwenye ufunguzi wa Maonesho ya 9 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yaliyoanza leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.Kulia ni Waziri wa Mawsiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa
 Mtaalamu wa Masuala ya Lishe kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Gaudensia Donati akimueleza jambo Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Jenista Muhagama (anayeonekana mikono),wakati walipotembelea banda la chuo hicho.
 Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa, akiangalia aina za panya wanazalishwa na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) katika Maonesho ya 9 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yaliyoanza leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee
 Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa, akimueleza jambo Makamu Mshauri wa Wanafunzi wa Shule ya Kimataifa ya Elimu iliyoko chini ya Chuo Kikuu cha Syansi na Teknolojia cha Huazhong cha nchini China, Annie Zhao wakati alipotembelea banda la chuo hicho
 Makamu Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Zanzibar, Profesa Idris Rai akiwaonesha jambo Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa (katikati) na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Jenista Muhagama, wakati walipotembelea banda la chuo hicho.
 Afisa Mitihani kutoka Baraza la Mitihani, Daniel Malemba akiwaeleza jambo baadhi ya wanafunzi waliotembelea banda la baraza hilo kwenye  Maonesho ya 9 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yaliyoanza leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.

 Afisa Uhusiano wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro Ally Sadi, akizungumza na baadhi ya wanafunzi waliotembelea banda la baraza hilo kwenye  Maonesho ya 9 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yaliyoanza leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.
 Afisa Mikopo Mwandamizi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu(HESLB ), Josephat Bwathondi, akitoa maelezo kwa baadhi ya wanafunzi waliotembelea banda la bodi hiyo kwenye  Maonesho ya 9 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yaliyoanza leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.

Mwanafunzi wa Mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Udaktari na Teknolojia (IMTU) akimpima ‘presha’ Emmanuel Suluba ambaye ni mmoja wa wanafunzi walitembelea banda la chuo hicho ambapo vipimo hivyo vinatolewa bure.
Picha na Hussein Makame-MAELEZO 

No comments:

Post a Comment