Thursday, April 17, 2014

JESHI LA POLISI LATAHADHARISHA WANANCHI KUWA MAKINI WAKATI WA SIKUKUU YA PASAKA



Tunapoelekea kipindi hiki cha sikukuu ya Pasaka, Jeshi la Polisi nchini, linatoa tahadhari kwa wananchi kuwa makini katika suala la usalama wa maisha na mali zao.
Uzoefu unaonyesha kwamba, katika kipindi kama hiki cha sikukuu kuna baadhi ya watu hupenda kutumia fursa hiyo kufanya vitendo vya uhalifu. Hata hivyo, Jeshi la Polisi katika mikoa yote limejipanga vizuri kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kuhakikisha kwamba hakuna vitendo vyovyote vya uhalifu vitakavyojitokeza na endapo vitajitokeza viweze kudhibitiwa kwa haraka

No comments:

Post a Comment