Friday, April 18, 2014

RAIS MSTAAFU ALI HASSAN MWINYI AWAONDOA HOFU WATANZANIA, MUUNGANO BADO NI IMARA



 Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Alhaj Ali Hassan Mwinyi akipokea maelezo kutoka kwa Afisa wa Bunge Bwana Patson Sobha, wakati alipowasili kwenye Banda la Bunge la maonesho ya maadhisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanzania yanayoendelea katika Viwanja Vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam. Maonesho hayo yatakayofikia kilele siku ya Jumamosi Aprili 19, ikiwa ni maandalizi ya siku kuu ya Muungano ambayo huherekewa Aprili 26 kila mwaka.
Rais Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi akikabidhiwa  zawadi ya vitabu na nyaraka mbalimbali za Bunge na Bi. Devotha George alipotembelea banda la Ofisi ya Bunge kwenye Maonesho ya maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam.
ais Msaafu wa awamu ya pili Ali Hassani Mwinyi akikabidhiwa nyaraka na Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Charles Chach,zenye ujumbe wa shughuli zinazofanywa na Mamlaka hiyo wakati alipotembelea katika banda la Mamlaka hiyo kujionea shughuli zinazofanywa na Mamlaka katika  Maadhimisho ya Miaka 50 ya sherehe za 
Muungano yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. 
Rais  mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassani Mwinyi  akimsikiliza kwa makini Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Charles Chacha wakati alipotembelea katika banda la Mamlaka hiyo  katika Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment