Saturday, April 19, 2014

WASHIRIKI WA KLINIKI YA AIRTEL RISING STAR KUTUA JIJINI DAR JUMATATU WIKI IJAYO



 Meneja uhusiano wa  Airtel Tanzania Jackson Mbando akiongea na waandishi wa Habari wakati wa kutangaza Kliniki ya Kimataifa ya mpira wa soka ya Manchester United ambayo itafanyika Jijini Dar es Salaam April 23-27 chini ya wakufunzi kutoka Klabu ya Manchester United. Kushoto ni Rais wa shirikisho la mpira wamiguu nchini (TFF) Jamal Malinzi. Iliofamyika jijini Dar-es-Salaam leo.
Rais wa shirikisho la mpira wamiguu nchini (TFF) Jamal Malinzi  akiongeana na waandishi wa habari wakati wa kutangaza Kliniki ya Kimataifa ya mpira wa soka ya Manchester United ambayo  itafanyika Jijini Dar es Salaam April 23-27 chini ya wakufunzi kutoka Klabu ya Manchester United. Kulia ni meneja uhusino wa Airtel Tanzania Jackson Mbando.
**********************************

·      Ni kutoka nchi 12 Afrika
·      Waziri Bernard Membe mgeni rasmi siku ya ufunguzi
·      Kliniki kuendeshwa na makocha kutoka Manchester United

 Wachezaji wa soka chini ya umri wa miaka 17 kutoka nchi 12 barani Afrika wanatarajiwa kuwasili jijini Dar es Salaam Jumatatu Aprili 21 kushiriki kliniki ya soka ya kimataifa.  Hii ni mara ya pili Tanzania imepewa heshima ya kuwa mwenyeji wa kliniki ya kimataifa baada ya ile iliyofanyika kwenye uwanja wa wa kisasa wa Taifa mwaka 2011.

Kliniki ya mwaka huu itakayofanyika kwenye uwanja wa Azam, Chamazi, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam inakutanisha wachezaji chipukizi, wasichana na wavulana, kutoka nchi zaKenya, Uganda, Malawi, Sierra Leone, Burkina Faso, Chad, Congo Brazzaville, DRC, Niger, Madagascar, Gabon, Seychelles na mwenyeji – Tanzania.

Mafunzo hayo ya siku tano mfululizo chini ya makocha wazoefu kutoka klabu maarufu duniani ya Manchester United yana lengo la kuwapa vijana mbinu mbalimbali za kisoka hasa katika eneo la ushambuliaji.

No comments:

Post a Comment