Saturday, April 12, 2014

WAVUVI KIBIRIZI MKOANI KIGOMA WATOA KILIO CHA KERO ZA LESENI NA KODI KWA KINANA

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisoma bango lenye ujumbe wa kulalamikia kodi kubwa  wanazotozwa wavuvi wadogowadogo wa Kibirizi,Kigoma.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Kibirizi mkoani Kigoma ambao wanakilio cha kutozwa kodi kubwa, kuvamiwa na majambazi wakati wa uvuvi.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akisalimiana na Mama Mawazo Rashid Mawala mkazi wa Ujiji Kigoma ,Katibu Mkuu alikuwa akitembea kwenye njia iliyotumika na Watumwa ambapo kuna miembe yenye umri zaidi ya miaka 150.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Mzee Masoud Mwinyi Chande kwenye mnara wa kumbukumbu ya nyumba ya kwanza ambayo Mwalimu Julius Nyerere alifikia Ujiji wakati akifanya harakati za kutafuta Uhuru, Nyumba hiyo inasemekana Mwalimu Nyerere alifika akiongozana na Suleiman Takadili na Bibi Titi Mohamed.

No comments:

Post a Comment