Sunday, April 13, 2014

MAKAMU WA RAIS, DKT. BILAL, WAZIRI MAGUFULI, KAMANDA KOVA NA MKUU WA MKOA WA DAR, MECKY SADICK, WANUSURIKA AJALI YA HELKOPTA DAR

Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa Helkopta ya JWTZ, iliyokuwa imewabeba viongozi, akiwamo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Kamanda wa Kanda Maalum ya Polisi, Suleiman Kova, Waziri wa Ujenzi, John Pombe Magufuli, Mkuu wa Mka wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick, imeangu wakati ikijaribu kuruka kwenye uwanja wa Jeshi Air wing.

Helkopta hiyo ilikuwa ikiwapeleka viongozi hao kukagua athali za mafuriko katika maeneo mbalimbali ya jiji pamoja na mkoa wa Morogoro, huku ikiwa pia na baadhi ya maafisa wengine. 

Katika ajali hiyo watu wote wametoka salama, isipokuwa baadhi wametoka wakiwa namajeraha katika sehemu za miili yao.

No comments:

Post a Comment