Friday, April 11, 2014

WAMILIKI WA VYOMBO VYA HABARI WATAKIWA KUHESHIMU TAALUMA YA HABAR





Mtaalam wa Sauti na Taa wa Clouds Media Cyprian Kisheto akimueleza jambo Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene wakati wa Ziara ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari kwenye Vyombo vya habari.

Picha na Hassan Silayo- Maelezo


Na Jovina Bujulu-MAELEZO
Wamiliki wa Vyombo vya habari nchini wametakiwa kutumia waandishi wa habari wenye Taaluma ya habari ili kuweza kuilinda taaluma hiyo.
Wito huo umetolewa na Mkurungenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene wakati wa Ziara ya Kikazi aliyoifanya katika Kituo cha Clouds Media leo Jijini Dar es Salaam.
Mwambene Alisema kuwa kumekuwa kukiongeza kwa wimbi la wanahabarti wasio na taalum hali inayosababisha kudharaulika kwa taalum hiyo.
“me napenda kuwaasa wamiliki wa vyombo vya habari kuendelea kusisitiza uajiri wa watu wenye taalum husika na wale waliosomea masuala haya ya uandishi wa habari ikiwa ni njia ya kuimarisha na kuilinda taaluma hii” Alisema Mwambene.
Akizungumzia kuhusu waandishi wasio uwezo Mhariri Mkuu wa habari Bi. Joyce Shebe alisema kuwa baadhi ya vyuo vya habari nchini vimekuwa vikizalisha waandishi wasiokidhi viwango.
Aidha aliongeza kuwa ofisi yao imekuwa na utaratibu wa kuwaendeleza wafanyakazi kwa lengo la kuwajendgea uwezo wa utendaji kazi katika Tasnia ya Habari nchini.
Ili kuhakikisha Tasnia ya Habari inakuwa wadau wa habari nchini wameombwa kuendelea kuishauri serikali katika masuala mbalimbali yatakayosaidia kuimarisha Tasnia hiyo

No comments:

Post a Comment