Saturday, April 12, 2014

MAMA SALMA KIKWETE AFUNGUA KONGAMANO KWA WANAFUNZI WA KIKE WA VYUO VIKUU NA SEKONDARI HUKO DODOMA

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akiwasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma na kupokewa na Mkuu wa Mkoa huo Dr. Rehema Nchimbi tarehe 11.4.2014.

 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akikaribishwa kwa shamrashamra za kwaya na matarumbeta wakati alipotua kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma kwa ziara ya siku tatu mkoani humo.


Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akipanda mti eneo la jengo la utawala wa Chuo Kikuu cha Dodoma wakati alipotembelea chuoni hapo kwa ajili ya kufungua rasmi kongamano la Mustakabali wa mtoto wa kike katika mazingira ya sasa kwa wanafunzi  wa kike wa vyuo vikuu vilivyopo Dodoma na Morogoro. Kongamano hilo lilifanyika katika ukumbi wa Chimwaga  tarehe 12.4.2014.


 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akikaribishwa ukumbini na wanafunzi wa kike waliojawa na furaha na hamasa kubwa

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akishiriki kucheza kwa nderemo na vifijo na wanafunzi wa kike wa vyuo vikuu mbalimbali vya Dodoma na Morogoro wimbo uitwao  ..”wanawake na maendeleo..” mara baada kuingia ukumbini. Mama Salma alikuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa kongamano la mustakabali wa mtoto wa kike katika mazingira ya sasa.





Kaimu Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma  Profesa  Herman Mlacha akimkabidhi Mke wa Rais Mama Salma Kikwete zawadi ya ramani ya Tanzania yenye kuonyesha pia picha ya Chuo Kikuu cha Dodoma  mara baada ya ufunguzi wa kongamano hilo tarehe 12.4.2014.



  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia mamia ya wanafunzi  wa kike kutoka vyuo vikuu waliofurika katika ukumbi wa Chimwaga huko Dodoma tarehe 12.4.2014.

No comments:

Post a Comment