Tuesday, April 15, 2014

TAASISI YA KIVULINI YAANZA VIKAO VYA TATHMINI YA UTENDAJI KAZI KWA WASAIDIZI WA KISHERIA KATIKA WILAYA ZA SENGEREMA, MAGU, MISUNGWI NA KWIMBA MKOANI MWANZA.

 Taasisi isiyo ya kiserikali inayojishughulisha na kutetea haki za Wanawake, KIVULINI, yenye makao makuu jijini Mwanza imeanza kufanya vikao vya tathmini ya utendeji kazi wa wasaidizi wa kisheria kwa robo mwaka wa pili katika ngazi za wilaya chini ya mradi wa msaada wa kisheria na haki za binaadamu.

Vikao hivyo vilivyoanza leo katika wilaya ya Sengerema kwa kukutana na wasaidizi wa kisheria 25 wanaofanya kazi ya kutatua migogoro ya kisheria kwa kutoa ushauri na elimu ya kisheria katika vijini vya wilaya ya sengerema, vikao hovyo vinatarajiwa kufanyika pia katika wilaya ya Magu, Misungwi na Kwimba zote zipo ndani ya mkoa wa Mwanza.

Kivulini kupitia mradi wa msaada wa kisheria imetekeleza shughuli mbalimbali kwa lengo la kuisaidia jamii kupata uelewa wa haki zao za kisheria na pia kundeleza uwepo wa elimu na ushauri wa kisheria katika maeneo ambayo mradi unatekelezwa.

Na juhudi kubwa imewekwa katika kuwajengea uwezo wasaidizi wa kisheria kwa sabaabu wasidizi wa kisheria wanaitajika ili kuiwezesha jamii kuweza kupata haki hasa wale walioko pembezoni mwa miji. Na kwa kupitia umoja wa wasaidizi wa kisheria wataweza kutoa elimu kwa wanajamii ili waweze kujua haki zo za kisheria na matatizo yanayopelekea uvunjifu wa haki na kuchukua hatua.

Kivulini Iliwezesha uundwaji wa umoja wa vikundi vinne vya  wasaidizi wa kisheria katika wilaya ya kwimba, Misungwi, Sengerema na Magu  na umoja huo unaundwa na jumla ya wajumbe 25 kwa kila kikundi ambao walipata mafunzo ya wasaidizi wa kisheria kwa kutumia mtaala wa chama cha wanasheria Tanganyika.
Wasaidizi wa kisheria wameendelea kutoa huduma ya ushauri wa kisheria kwa wanajamii  hasa kwa makundi yasiyojiweza katika kata 52, kwa kipindi cha robo mwaka ya pili wasaidizi wa kisheria wamepokea mashauri 129 kwa ujumla katika mashauri hayo yaliyokamilika ni mashauri 60 yaliyotolewa rufaa ni 43 na yanayoendelea nimashauri 43, ukilinganisha na robo mwaka ya kwanza ambapo mashauri 200 yalipokelewa ambayo inafanya jumla ya mashauri 329 yaliyopokelewa na wasaidizi wa kisheria.
KIVULINI ni Shirika linalojishughulisha na Kutetea Haki za Wanawake na Wasichana lenye makao yake makuu jijiini Mwanza tangu mwaka 1998

No comments:

Post a Comment