Wednesday, May 28, 2014

BALOZI SEIF IDDI AJIPONGEZA NA WIZARA YAKE KWA KUPITISHWA KWA BAJETI.

                 Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Baraza la Wawakilishi wa mwanzo kulia Mh. Saleh Nassor Juma akiwa pamoja na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Abdulla Mwinyi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed wakijipatia mlo kwenye dhifa maalum iliyoandaliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Nyumbani kwake Mazizini.
  Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Mh. Ali Mzee Ali akipata msosi katika dhifa maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya kuwapongeza watendaji wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar baada ya kumaliza kupitishwa kwa bajeti ya wizara hiyo.
 Mkurugenzi Idara ya Mipango, Sera na Utafiti OMPR – ZNZ Nd. Khatib  Said Khatib, Msaidizi wa Mhe. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Iddi pamoja na Mwakilishi wa Jimbo la Micheweni Mh. Subeti Khamis wakiwa miongoni mwa watu walioshiriki dhifa hiyo.

 Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Dr. Khalid Salum Moh’d akitoa shukrani kwa niaba ya watendaji wa Ofisi hiyo baada ya kumaliza dhifa maalum waliyoandaliwa watendaji hao.
 Baadhi ya watendaji wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar walioshiriki dhifa maalum ya kupongezana baada ya kazi nzito ya Bajeti ya Wizara yao.   
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwapongeza watendaji wa Ofisi yake kwa kazi kubwa waliyoifanya kumaliza salama bila ya vikwazo bajeti ya Wizara yao.
 Msanii Matona Issa Matona akifanya vitu vyake wakati wa burdani maalum iliyohusika katika dhifa waliyoandaliwa watendaji wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.Kulia kwake ni wake wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Pili Juma mIddi na Mama Asha Suleiman Iddi pamoja na mfanyakazi wa Wizara ya Nchi –OMPR – ZNZ Bi. Khabiba Janja wakiserebuka kwenye burdani hiyo.

  Mwakilishi wa Kuteuliwa wa Baraza la Wawakilishi Mh. Ali Mzee Ali aliyevaa suti nyeusi pembeni yake akifuatiuwa na Waziri wa Nchini Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed wakitunza wakati wa burdani maalum iliyopigwa kwenye dhifaa ya watendaji wa Ofisi hiyo. Watendaji wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na wageni waalikwa wakisakata ngoma wakati wa dhifa maalum ya watendaji wa Ofisi hiyo.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akimkabidhi zawadi maalum ya Shilingi  Laki 500.000/-Kiongozi wa Kikundi cha Taarab asilia cha Akheri Zamani Msanii Matona Issa Matona baada ya kutumbuiza kwenye dhifa maalum ya Ofisi hiyo iliyofanyika nyumbani kwa Balozi Seif Mazizini.
Balozi Seif akiagana na baadhi ya wasanii wa Kikundi cha taarab asilia cha Akheri Zamani baada ya kumaliza kazi yao ya burdani kwenye dhifa ya watendaji wa Ofisi yake.

Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed amewashukuru Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Baraza la Wawakilishi kwa mapendekezo yao yaliyoiwezesha Bajeti ya Ofisi na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kupita bila ya vikwazo.
Mapema Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Dr. Khalid Salum Mohd kwa niaba ya wafanyakazi wa Wizara hiyo amempongeza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Familia yake kwa uamuzi wake wa kuwa pamoja na watendaji wake katika kubadilishana mawazo baada ya kazi nzito ya Bajeti ya Wizara hiyo.
Dhifa hiyo iliyojumuisha watendaji wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Baraza la Wawakilishi na baadhi ya watendaji wake pamoja na familia ya Makamu wa Pili wa Rais iliongozwa na muziki laini uliokuwa ukiporomoshwa na Kikundi mahiri cha Muziki wa Taarabu asilia cha Akheri Zamani.                           

Watendaji wa Wizara ya nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wana wajibu mkubwa wa kuhakikisha mawazo na maagizo yote yaliyotolewa na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi katika kikao chao kinachoendelea wanayatekeleza kwa nguvu zao.
Utekelezaji huo ndio kigezo pekee kitakachoashiria Wizara hiyo inafikia lengo liliomo katika mpango wake wa  kazi za kawaida na maendeleo iliyouwasilisha kwenye Baraza la Wawakilishi wa mwaka 2014/2015 na kupitishwa na Wajumbe wa Baraza hilo bila ya vikwazo wala kubadilika.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alitoa agizo hilo katika dhifa maalum aliyowaandalia watendaji wa Ofisi yake hapo nyumbani kwake Mazizini nje kidogo ya Mji wa Zanzibar baada ya kazi nzito waliyoifanya ya kuandaa Bajeti ya Wizara hiyo na hatimae kupitishwa na Baraza la Wawakilishi bila ya matatizo.
Balozi Seif alisema kilichokuwa kikiwakabili watendaji hao sio kazi rahisi lakini umoja na mshikamano wao wa pamoja ndio  siri halisi iliyochangia kufanikisha kazi hiyo ambayo inafaa kuigwa na Wizara nyengine za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.


Othman Khami Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
28/5/2014.

No comments:

Post a Comment