Friday, May 23, 2014

RAIS KAGAME AFUNGUA RASMI MKUTANO WA MWAKA WA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA (AfDB) UNAOFANYIKA JIJINI KIGALI RWANDA.


Kikundi cha Ngoma za asili cha Bollet Nationol – URUKEREREZA cha jijini Rwanda kikitumbuiza wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika unaofanyika Rwanda.


 Mh.Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum na Washiriki mbalimbali wa Mkutano wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika mara baada ya ufunguzi wa Mkutano huo uliofunguliwa na Mh.Paul Kagame katika ukumbi wa Mount Karisimbi Jijini Kigali Rwanda.
Baadhi ya Viongozi Wakuu wa Afrika waliohudhuria Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika ambao ulifunguliwa na Mh.Rais wa Rwanda Paul Kagame. Mh.Kagame katika hotuba yake alisisitiza kuzijengea uwezo sekta binafsi ili Afrika iweze kufikia uchumi wa kati kwa kipindi cha Miaka 50 ijayo. Aidha katika kufikia lengo hilo Rais Kagame alisema hatuna budi Afrika kuachana na Migogoro na kutekeleza kwa vitendo makubaliano yanayoafikiwa na Viongozi wa Afrika  ili kujenga uchumi imara kwa vizazi vijavyo.

No comments:

Post a Comment