Tuesday, May 27, 2014

CAMEROON YASHINDA LICHA YA MAJERAHA.

Cameroon yashinda ingawa tatizo la majeraha laongezeka.


Nahodha wa Cameroon Samwel Eto’o katika mechi ya kujipima nguvu ambayo The indomitable Lions iliishinda Macedonia mabao 2-0 nchini Austria.
Cameroon yashinda ingawa tatizo la majeraha laongezeka.
Etoo alipumziswa huku timu hiyo ikiendelea kukumbwa na majeraha zaidi kabla ya kombe la dunia.

Jean-Eric Maxim Choupo-Moting baadae akaongeza bao la pili.Mshambulizi huyo wa Chelsea hakuchezeshwa kutokana na jeraha la goti, huku Cameroon ikimpoteza mshambulizi mwingine Pierre Webo kutokana na jeraha siku ya Jumatatu punde baada ya kufunga.

Kipa Charles Itandje, mlinzi Jean-Armel Kana-Biyik na viungo Edgar Salli, Jean II Makoun na Stephane Mbia wote wanauguza majeraha tofauti.
Cameroon bado wana mechi za kujipima nguvu dhidi ya Paraguay, Ujerumani na Moldova kabla ya kombe la dunia.

No comments:

Post a Comment