Saturday, May 31, 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHANI MSIBA WA BABA YAKE ROSTAM AZIZI JIJINI DAR LEO

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rostam Azizi, wakati alipofika nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo Mei 31, 2014 kwa ajili ya kumpa pole kwa kufiwa na Baba yake mzazi aliyefariki katikati ya wiki hii.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (katikati) akijumuika na waombolezaji waliofika  nyumbani kwa Rostam Azizi, Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo Mei 31, 2014 kwa ajili ya kumpa pole kwa kufiwa na Baba yake mzazi aliyefariki katikati ya wiki hii.
 Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa, akitoa mawaidha wakati wa dua maalum iliyofanyika nyumbani kwa Rostam Azizi Oysterbay kumuombea Baba mzazi wa Rostam, aliyefariki katikati ya wiki hii.
Baadhi ya waombolezaji walioshiriki dua hiyo maalum nyumbani kwa Rostam Azizi.

No comments:

Post a Comment