Friday, May 30, 2014

PIGO TENA!!!! BONGO MOVIE :MUONGOZAJI WA FILAMU NA VIPINDI MBALI MBALI VYA TELEVISHENI HAPA NCHINI,GEORGE TYSON (PICHANI) AMEFARIKI DUNIA.

TAARIFA ZILIZOTUFIKIA KUTOKA MKOANI MOROGORO ,ZINAELEZA KUWA ALIEKUWA MUONGOZAJI WA FILAMU NA VIPINDI MBALI MBALI VYA TELEVISHENI HAPA NCHINI,GEORGE TYSON (PICHANI) AMEFARIKI DUNIA.

GEORGE TYSON AMEFIKWA NA MAUTI HAYO MAJIRA YA SAA 12 JIONI BAADA YA KUPATA AJALI MBAYA SANA KUTOKANA NA GARI WALIOLOKUWA WAKISAFIRIA KUTOKA MKOANI DODOMA KUJA DAR ES SALAAM,WAKITOKEA KWENYE HAFLA YA KUADHIMISHA MIAKA MIWILI YA KIPINDI CHA TELEVISHENI CHA THE MBONI SHOW,KUPINDUKA MARA KADHAA KUTOKANA NA KUPASUKA KWA MIPIRA MIWILI (MATAIRI) YA GARI HIYO AINA YA TOYOTA NOAH.

AJALI HIYO IMETOKEA MAJIRA YA SAA MOJA JIONI,ENEO LA GAIRO MKOANI MOROGORO.

NDANI YA GARI HILO KULIKUWA NA WATU NANE,KATI YAO NI WAPIGA PICHA WA SHOW HIYO AMBAO NAO HALI ZAO NI MBAYA KUTOKANA NA KUUMIA MAENEO MBALI MBALI YA MIILI YAO NA KUKIMBIZWA HOSPITALI YA RUFAA YA MOROGORO KWA MATIBABU.
Screen Shot 2014-05-31 at 3.46.30 AM
Dj Choka ambae kwa sehemu kubwa alikua kwenye safari moja ya Dodoma na Marehemu George Tyson, ameandika kwenye http://djchokamusic.com/ kwamba Marehemu alikuwa yupo kijiji cha Chilonwa Chamwino kwenye utoaji wa madawati katika shule ya msingi Chaula iliyopo Dodoma.

Baada ya kumaliza shughuli hii huku akiwa kama producer wa The Mboni Show mauti yalimkuta majira ya saa 12 jioni ikiwa ni saa 4 tu toka tuanze safari ya kurudi Dar es Salaam maeneo fulani hivi kama unataka kukaribia GAIRO mjini.
Kwenye gari walikuwa watu 8 ila yeye pekee ndio aliyepoteza maisha ila wengine wamepata majeraha mwilini akiwemo dereva wa gari hilo ambapo kwa sasa mwili wa marehemu umehifadhiwa hapa Morogoro katika hospital ya mkoa Morogoro baadae asubuhi safari ya kurudi Dar es Salaam itaanza.
Screen Shot 2014-05-31 at 3.46.12 AM
Screen Shot 2014-05-31 at 3.46.38 AM
Screen Shot 2014-05-31 at 3.46.50 AM
Kwenye hii safari, George Tyson aliambatana na mtangazaji Mboni Masimba wa The Mboni show.
Screen Shot 2014-05-31 at 3.46.58 AM
Screen Shot 2014-05-31 at 3.47.07 AM
Tutaendelea kupeana taarifa kadri zitakavyokuwa zikitufikia.


No comments:

Post a Comment