Saturday, May 24, 2014

REAL MADRID MABINGWA LIGI YA MABINGWA WAWATANDIKA ATLETICO MADRID MABAO 4-1


 Golikipa wa Real Madrid, Iker Casillas, (katikati) akinyanyua Kombe la Ligi ya Mabingwa baada ya mechi ya Fainali na Atletico Madrid iliyochezwa jana usiku kwenye Uwanja wa Luz huko Lisbon. Katika mchezo huo Real Madrid ilishinda mabao 4-1. 
 Mshambuliaji wa Real Madrid,  Sergio Ramos, (katikati) akishangilia na wachezaji wenzake baada ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Atletico Madrid katika fainali ya Ligi ya Mabingwa uliochezwa jana usiku.
 Mshambuliaji wa Real Madrid, Christiano Ronaldo, (kushoto chini) akilalamika kwa mwamuzi Bjorn Kuipers, wakati wa mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Atletico Madrid, uliopigwa jana usiku huko Lisbon. Madrid ilishinda 4-1 dhidi ya atletico.
Karim Benzema, (kulia) akiwania mpira na Miranda wa Atletico, wakati wa mchezo huo.

No comments:

Post a Comment