Saturday, May 24, 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWAELEZA WASOMI JAPAN UMUHIMU WA VITEGA UCHUMI KWA MAENDELEO YA AFRIKA



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa muhadhara katika Chuo Kikuu cha Taaluma ya Sera 'GRIPS' wakati alipoalikwa kwenye muhadhara huo uliofanyika chuoni hapo Jijini Tokyo Japan, jana Mei 23, 2014.
  Baadhi ya wanachuo kutoka mataifa mbalimbali wa Chuo hicho waliohudhuria Muhadhara huo, wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati alipokuwa akitoa muhadhara. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini Japan, waliohudhuria Muhadhara huo baada ya kumalizika kwa muhadhara huo katika Chuo Kikuu cha Taaluma ya Sera 'GRIPS' Jijini Tokyo Japan, jana.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya wanachuo Watanzania, wanaosoma katika Chuo hicho baada ya kumalizika kwa Muahadhara huo jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanachuo Watanzania wanaosoma katika Chuo hicho cha  Taaluma ya Sera 'GRIPS' Jijini Tokyo Japan, jana Mei 23, 2014, baada ya kumalizika kwa muhadhara huo. 
************************************************************
*DKT. BILAL AWAELEZA WASOMI JAPAN UMUHIMU WA VITEGA UCHUMI KWA MAENDELEO YA AFRIKA
Na Mwandishi Maalum, Tokyo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal amesema nchi zinazoendelea hususan za Kiafrika bado zinahitaji uwekezaji zaidi vitega uchumi kutoka nje  (FDIs) ili kupata maendeleo ya haraka na  kuondokana na umaskini.
Dkt. Bilal ameyasema hayo leo (Mei 23, 2014) wakati akitoa muhadhara kuhusu Mtazamo wa Nchi Zinazoendelea  na  Changamoto za Uwekezaji Vitega Uchumi  vya Nje na Hatma yake katika Kuondoa Umasikini kwa  kutumia  mfano wa Tanzania ulioandaliwa na  Taasisi ya Uchanganuzi wa  Sera (GRIPS)  mjini  Tokyo.
Alisema Afrika inahitaji misaada zaidi itakayosadia kukuza teknolojia itakayowawezesha Waafrika kuvuna  maliasili ambazo hazijavunwa. Aliongeza kuwa hii ndiyo njia pekee itakayoliwezesha Bara la Afrika kuongeza mapato na kuchangia maendeleo ya haraka kwa wananchi wake.
Alisisitiza  kuwa uwekezaji unaohitajika zaidi ni katika sekta za  za madini, mafuta na gesi, kilimo na vyanzo vingine vya nishati kama vile nishati ya jua na upepo. Alisema sekta hizo ndizo zinazohitaji teknolojia ya kisasa kutoka mataifa yaliyoendelea ili kurahisisha uvunaji wake.

Wakichangia hoja hiyo, wanafunzi wa chuo hicho walihoji namna Tanzania inavyojiandaa kuhakikisha upatikanaji wa mafuta na gesi hauwezi kuathiri amani na utulivu wa nchi yetu. Makamu wa Rais aliwaeleza kwamba utafutaji, uchimbaji na usambaji unafanyika katika misingi ya uwazi ili Serikali na  kila mwananchi aelewe ni kwa namna gani atakavyonufaika na rasimiali hiyo.

No comments:

Post a Comment