Wednesday, May 28, 2014

WANACHAMA WA SIMBA WAFUNGA BARABARA YA MSIMBAZI, DAR KUSHINIKIZA WAMBURA ARUDISHWE KWENYE ORODHA YA WAGOMBEA

 Mashabiki wa Timu ya simba wakijikusanya nje ya jengo la klabu hiyo kongwe kupinga wambura kuondolewa kwenye uchaguzi unakuja hivi karibuni

 Hapa mashabiki wakizidi kujikusanya kwa wingi mchana huu.

 Wanachama wa simba wakiwa wamelizunguka Jengo la klabu yao mchana huu kupinga kuondolewa kwa wambura kwenye uchaguzi wa klabu hiyo.
 Wanachama wa Simba wakipiga kelele nje ya jengo la klabu yao hiyo wakitaka wapewe ufafanuzi wa kina kwanini wambura ametolewa kwenye uchaguzi unaokuja.
 Mmoja wa wanachama wa Simba akiongea na mamia ya wanachama nje ya jengo la klabu hiyo kutaka wambura arejeshwe mara moja kwenye orodha ya wagombea.
 Hapo mmoja ya wanachama waliojikusnya akiwatuliza wanachama wenzake ili waweze kupatamaelezo.
 Polisi wakiwa wamefika eneo la klabu ya simba ili kuimarisha ulinzi na kuwataka wanachama wa simba kutulia ili wapate majibu kwa kamati ya uchaguzi.
 Mamia ya wanachama wa simba wakiwa nje ya jengo la simba mchan huu.


Mamia ya wapenzi na washabiki wa klabu kongwe ya mpira wa miguu hapa nchini Simba leo mchana wamejikusanya kwa wingi na kupinga Michael Wambura kuondolewa kwenye orodha ya wagombea kwenye uchaguzi unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni. Wanachama hao ambao walizunguka jengo hilo na kutaka wapewe sababu za msingi kwanini mgombea wao Wambura ameondolewa huku wakitaka kufanya vurugu lakini vyombo vya usalama waliwahi kufika eneo la tukio na kuweza kuwatuliza wanachama hao.

No comments:

Post a Comment