Friday, May 30, 2014

KAMPENI KABAMBE BARANI AFRIKA KUKOMESHA NDOA ZA UTOTONI.

Baadhi ya jamii afrika huoza watoto wao wadogo kwa sababu za kifedha
Umoja wa Afrika umeanzisha kampeini kabambe barani Afrika kusitisha ndoa za watoto wadogo.
Kampeini hiyo ilizinduliwa mjini Addis Ababa katika makao makuu ya umoja huo .Inakisiwa kuwa asili mia tisini ya nchi zinazoathiriwa na ndoa hizi ni za AfrikaWataalamu wameonya kuwa ndoa za watoto wadogo zinakatiza ujana wa wasichana zaidi ya milioni kumi na saba, au mmoja kati ya wasichana watatu barani Afrika.
Watetezi wa haki za watoto, wanasema kuwa ndoa za watoto zinakiuka haki za msingi za wasichana kama vile elimu kwasababu wakiolewa wanalazimishwa kuacha shule na kuwahudumia waume zao.
Pia kuna hofu kubwa za kiafya kwa kila msichana mwenye umri mdogo anayepata mimba.
Baadhi wanasema kuwa wasichana hawa pia mara nyingi wanaishi kama wafungwa kwenye nyumba zao huku wakinyimwa ruhusa ya kutoka nje na huenda hata wanapigwa na kunyanyaswa.
Barani Afrika, nchi inayoaminika kuwa na idadi kubwa zaidi ya wasichana wadogo wanaoolewa, mara nyingi kwa lazima, ni Niger ambayo imefikia asilia mia sabini na tano.

Inafuatiwa kwa karibu zaidi na Jamhuri ya Afrika ya Kati na Chad.

No comments:

Post a Comment