Monday, May 27, 2013

*TWIGA CEMENT YAZINDUA MRADI WA UJENZI WA BARABARA YA TEGETA -WAZO


  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Saruji ya Twiga (TPCC), Pascal Lesoinne (wa pili kushoto) Diwani wa Kata ya Wazo, John Moro (kushoto kwake) wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Wazo Misikiti na PK Tegeta itakayojengwa na kampuni hiyo. Hafla ya uzinduzi ilifanyika Wazo Hill nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Wengine kutoka kulia ni Meneja Huduma za Jamii wa TPCC, Natasha D’Souza, Mkuu wa Rasilimali Watu wa kampuni hiyo, Jayne Nyimbo na Mwenyekiti wa Mtaa wa Wazo, Mtuzya Abdallah ,Mtuzya. Ujenzi huo utagharimu shs milioni 175. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Saruji ya Twiga (TPCC), Pascal Lesoinne (katikati) akibadilishana mawazo na Diwani wa Kata ya Wazo, John Moro muda mfupi kabla ya hafla ya uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Wazo Misikiti na PK Tegeta itakayojengwa na kampuni hiyo. Hafla ya uzinduzi ilifanyika Wazo Hill nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Kulia ni Ofisa Mtendaji wa kata hiyo, Ibrahim Mabewa. Ujenzi huo utagharimu shs milioni 175. 
Baadhi ya wananchi waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Wazo Msikiti na Tegeta PK itakayojengwa na kampuni ya Twiga Cement.

No comments:

Post a Comment