Thursday, May 30, 2013

MWILI WA MAREHEMU ALBERT MANGWAIR KUWASILI NCHINI TANZANIA JUMAMOSI.


Taarifa zilizotufikia hivi punde kutoka kwa kaka wa Marehemu Keneth Mangwea, zinaeleza kuwa,  
mwili wa marehmu mdogo wake, Albert Mangwea, unatarajia kuwasili 
nchini siku ya Jumamosi ya Juni 1, ukitokea nchini Afrika ya Kusini.

Aidha Keneth, amesema kuwa utaratibu wa shughuli zote za maziko ikiwa ni pamoja na kuaga mwili wa marehemuna kutoa 
heshima za mwisho kwa 
Msanii huyo nguli wa Muziki wa Kizazi kipya 
Tanzania zitatolewa 
baada ya kamati Uhusika 
na familia kupanga.

Kaa nasi na Endelea kupitia mtandao 
huu ili kupata taarifa kuhusu shughuli nzima ya msiba 
wa Ndugu yetu Albert mangwea, aliyefariki
Mei 28 Nchini Afrika ya Kusini

No comments:

Post a Comment