Wednesday, May 29, 2013

*REDD'S MISS TANZANIA AWATAKA REDD'S MISS SINZA 2013 KULINDA HESHIMA

 Miss Sinza na Miss Tanzania 2012-2013, Brigit Alfred (kulia) akizungumza na Warembo wanaotarajia kuwania Taji la Redd's Miss Sinza 2013, wakati alipowatembelea katika Kambi yao ya mazoezi jana katika Ukumbi wa Meeda Sinza na kuwafunda kuhusu mashindano hayo kuelekea shindano hilo linalotarajia kufanyika Juni 7,mwaka huu kwenye Ukumbi huo. Katika shindano hilo Viingilio vitakuwa ni Sh. 20,000 kwa VIP na viti vya kawaida ni Sh. 10,000. Shindano hilo limedhaminiwa na Mtandao wa www.sufianimafoto.com, Dodoma Wine, Chilly Willy Energy Drink, Clouds Media Group, CXC Africa, Saluti5 na Fredito Entertainment.
Miss Sinza na Miss Tanzania 2012-2013, Brigit Alfred (katikati) akipozi na warembo wanaowania Taji la Redd's Miss Sinza 2013, wakati alipowatembelea kwenye Kambi yao ya mazoezi katika Ukumbi wa Meeda Sinza.
***************************************
Na Mwandishi wetu
Redds Miss Tanzania 2012 ambaye pia ni Redds Miss Sinza, Brigitte Alfred amewataka warembo wanaowania taji la mwaka huu la kituo cha Sinza kutomuangusha  kwa kufauata nyayo zake katika shindano lililopangwa kufanyika Juni 8 kwenye ukumbi wa Meeda Club.

Brigitte alisema hayo juzi alipotembelea warembo wanaowania taji la mwaka huu katika kinyang’anyiro hicho kilichodhaminiwa na bia ya Redds Origional, Dodoma Wine, Clouds Media Group, Chilly Willy Energy Drink, Fredito Entertainment, CXC Africa, Saluti5.com na Sufiani Mafoto blog.

Alisema kuwa  warembo wa kituo hicho wanakazi kubwa ya kushinda taji hilo na baadaye Miss Kinondoni na Miss Tanzania kama yeye alivyofanya.

Alifafanua kuwa siri kubwa ya mafanikio ni kujituma na kuwa na nidhamu ya hali ya juu kwani hata yeye alifundishwa na matroni wa sasa, Mwajabu Juma na waandaaji ni wale wale.

“Sioni sababu ya kushindwa kufanya vyema katika mashindano haya, Redds Miss Sinza ndiyo inatetea taji la Miss Kinondoni na Miss Tanzania pia, hivyo macho ya wadau wote wa urembo yatakuwa kwenu na ndicho kitongoji kinachofunga mashindano ya ngazi ya chini, mnatakiwa kujituma na kuwafanya majaji kuwa na kazi ya ziada kumpata mshindi,” alisema Brigitte.

Alisema kuwa wadau wa masuala ya urembo wanaangalia Sinza mwaka huu itafanya nini baada ya mafanikio makubwa ya mwaka jana. “Sisi tumejenga  msingi mkubwa na kuleta heshima kwa wakazi wa Sinza, Kinondoni na Tanzania kwa ujumla, nanyi mna jukumu hilo,” alisema.

Mratibu wa mashindano hayo, Majuto Omary alisema kuwa maandalizi yamekwisha kamilika na kiingilio ni sh 10,000 kwa viti vya kawaida na shs 20,000 kwa viti vya VIP. Alisema kuwa wanakamilisha maandalizi ya burudani ya siku hiyo ambayo itakuwa ya aina yake.

No comments:

Post a Comment