Wednesday, May 29, 2013

BREAKING NEWZZ MSANII ALIYEDAIWA KUFARIKI DUNIA YU HAI M2 THE P

Marehemu Albert Mangwair akiwa na M2 the P.  

Taarifa za uhakika zilizothibitishwa kutoka nchini Afrika Kusini zinasema kuwa Yule Msanii M2 The P aliyekuwa na marehemu Albert Mangwair, aliyeripotiwa kufariki duni siku ya jana amezinduka rasmi leo mchana akiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi nchini Afrika ya Kusini.

Akizungumza moja kwa moja kwa njia ya Simu kutoka nchini Afrika ya Kusini, Mtangazaji wa Redio Clouds, Millad Ayo, katika kindi cha Jahazi, alisema kuwa msanii huyo alionekana kupoteza fahamu na kuzimia kwa siku nzima kiasi cha kuripotiwa kufariki dunia siku ya jana.

Aidha alisema kuwa Msanii huyo leo asubuhi alizinduka na kufumbua macho na kujaribu kuinuka, lakini alishindwa na kurudi kulala, huku akitaka kujaribu kuzungumza na wabongo wenzake waliofika Hospitalini hapo bila mafanikio.

Hadi Millad anaripoti habari hii, bado msanii huyo alikuwa hai na akionyesha matumani, huku ikielezwa Hospitalini hapo kuwa Ripoti kamili ya kifo cha Manwair, itatolewa rasmi leo usiku.

No comments:

Post a Comment