Monday, May 27, 2013

*MISS SINZA NA MISS TANZANIA 2012-2013 KUWAFUNDA WAREMBO WA REDD'S MISS SINZA KESHO

Na Mwandishi wetu, Dar
Redds Miss Tanzania, Brigitte Alfred ataanza kazi ya kuwafunda warembo wa Redds Miss Sinza leo Jumanne katika ukumbi wa Meeda Club uliopo Sinza. Reddds Miss Sinza imepangwa kufanyika Juni 7 kwenye ukumbi huo.

Muandaaji wa mashindano hayo, Majuto Omary alisema kuwa Brigitte ambaye anatokea kituo hicho na kushinda taji la Kinondoni na la Tanzania, atafika kwenye mazoezi hayo saa 10.00 jioni na kuanza kazi hiyo katika mashindano hayo yaliyodhaminiwa pia na Dodoma Wine, Chilly Willy Energy Drink, Clouds Media Group, CXC Africa, Saluti5, Sufiani Mafoto blog na Fredito Entertainment.

Majuto alisema kuwa mrembo huyo ambaye hivi karibuni alikuwa nchini Afrika Kusini, alisema kuwa lengo kubwa ni kuwapa ‘mbinu’ jinsi gani warembo wa mwaka huu wa kituo cha Sinza watakavyoweza kushinda taji la kituo hicho, Kinondoni na vile vile Tanzania.

“Tumebakiza muda mfupi sana kabla ya kufanyika kwa Redds Miss Sinza 2013, warembo wapo wengi na mwisho wa kupokea warembo wengine ni Juni Mosi, sisi ndiyo tunaofunga mashindano wa kanda ya Kinondoni na tunatoa fursa kwa warembo kujaribu bahati yao,” alisema Majuto.

Alisema kuwa Redds Miss Sinza 2013 ni zaidi ya burudani kwani wamejipanga kufanya mambo makubwa siku ya mashindano na baada ya mashindano.

 “Sisi hatuuishii kufanya mashindano na kuangalia mwakani, kuna fursa mbali mbali za warembo ikiwa kutafutiwa nafasi za kazi kama ilivyokuwa mwaka jana ambapo tulipewa ofa nafasi tano za kazi,” alisema.

No comments:

Post a Comment