Wednesday, May 29, 2013

*ZIARA YA RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN NCHINI CHINA

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiuliza suala kwa waongozaji na watoa maelezo katika sehemu za kihistoria zenye kumbukumbu nyingi,zinazopelekea wageni wa aina tofauti kutembelea katika mji huo wa Beinjing nchini China.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Uchumi wa Maendeleo Omar Yussuf Mzee,akibadilishana Hati ya saini ya Mikataba ya uhusiano wa biashara na Naibu Waziri wa Biashara wa China Liu Cigui,baada ya kutilianan saini katika ukumbi wa mikutano wa China World Hotel. 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifuatana na ujumbe wake wakitembelea sehemu mbali mbali za  Kihistoria zilizopo katika makumbusho ya Mji wa  Beijing nchini China akiwa katika ziara ya kiserikali.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifuatana na Mkewe mama mwamamwema Shein,katika viwanja vya Makumbusho ya Kihistoria nchini Nchini China pamoja na  ujumbe waliofuatana nao katika ziara ya kiserikali.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(wa tatu kusoto) pamoja na ujumbe aliofuatana nao akiuliza suala kwa waongozaji na watoa maelezo katika sehemu za kihistoria zenye kumbukumbu nyingi,zinazotembelea na wageni mbali mbali  katika Mji huo wa Beinjing nchini China,akiwa katika ziara ya Kiserikali ya siku saba. Picha na Ramadhan Othman,China.

No comments:

Post a Comment