Mwakilishi wa mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Fulgens Lisakatu (katika) akiakata utepe kuashiria uzinduzi wa miwani ya Kibo ambayo itamuwezesha mtanzania yeyote kuweza kupimamacho na kupewa miwani kwa gharama nafuu, (wapili kulia ) ni Rasi wa Chama cha wataalamu wa macho nchini (TOA) Frank Magupa (wapili kushoto) ni Ofisa Mkazi wa Shirika la Brien Holden Vision Institute hapa nchini Eden Mashayo, wakwanza kushoto ni mratibu wa mradi huo Rebecca Kasika.uzinduzi huo ulifanyika katika viwanja vya Free Market jijini Dar es Salaam.
Rais wa Chama cha Wataalamu wa Macho hapa nchini(TOA) Frank Magupa (kushoto)akiongea wakati wa uzinduzi wa miwani ya Kibo jijini Dar es Salaam, ambapo huduma za macho zitatolewa hospitali za manispaa za Ilala ,Kinondoni na Temeke .Wananchi watapata fursa ya kupima macho na kupewa miwani kwa bei nafuu ambayo kila mtu ataimudu .Katikati ni Ofisa Mkazi wa Shirika la Brien Holden Vision Institute hapa nchini Eden Mashayo
Mwakilishi wa mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Fulgens Lisakatu (katika) akisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa watoa huduma ya kupima macho wakati alipotembelea banda la Ilala Eye Centre
Rais wa Chama cha Wataalamu wa Macho hapa nchini(TOA) Frank Magupa (kushoto)akimwelezea ubora wa miwani ya Kibo Mwakilishi wa mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Fulgens Lisakatu katika hafla ya uzinduzi wa miwani ya Kibo
Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika uzinduzi wa miwani aina ya Kibo yenye gaharama nafuu kwa wananchi,sensa ya 2012 inaonyesha kuwa mkoa wa Dar es Salaam,unawakazi zaidi ya Miliono Nne, na takwimu ya zilizotolewa na Mratibu wa Afya wa Dar es Salaam,kuanzia mwaka 2010 hadi 2013 zinaonyesha kuwa jumla ya wananchi 39,863. Wanaishi na ugonjwa wa Macho. Shirika la Holden Vision Institute na Taassisi ya wanaoptometria hivi karibuni walizindua miwani aina ya Kibo ambayo gaharama yake ni nafuu
Mwakilishi wa mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Fulgens Lisakatu akiongea na wananchi waliohufika katika uzinduzi wa miwani ya Kibo
Ofisa Mkazi wa Shirika la Brien Holden Vision Institute hapa nchini Eden Mashayo ,akiongea kuhusioana na utoaji wa huduma za kupima macho na kupewa miwani ya Kibo
Wafanyakazi wa Shirika lisilo la kiserikali la Brien Holden Vision Institute wakiwa ,katika picha ya pamoja na mgeni rasmi ,Mwakilishi wa mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Fulgens .Baada ya kumalizika kwa uzinduzi wa miwani ya Kibo , uliofanyika katika viwanja vya Free Market jijini Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment