Tuesday, April 8, 2014

JUMUIYA YA WAZAZI CCM MKOA WA MOROGORO WASISITIZA SERIKALI MBILI, WAVUNA WANACHAMA WA KUTOSHA


 Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Morogoro  Mh Abdalah Shaweji Akisikiliza kwa Makini Taarifa za Chama cha Mapinduzi alipowasili wilayani Mvomero kweny Maadhimisho ya Sherehe za Siku ya Wazazi Mkoani Morogoro. Katibu wa Jumuiya Hiyo alifanya Shuguli Mbalimbali Ikiwemo Kupanda miti Kufungua Mashina ya Chama cha Mapinduzi Pamoja na Kukabishi kadi za Uwanachama ambapo Jumla ya Wanachama 150 walijiunga na umoja wa wazazi.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Morogoro  Mh Abdalah Shaweji Akisaini Kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Ofisi za CCM Wilaya ya Mvomero
Wajumbe wa Kmatai ya Utekelezaji wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Morogoro Wakisaini kitabu cha wageni kwenye Ofisi za CCM Wilaya ya Mvomero.

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Morogoro  Mh Abdalah Shaweji aliyevaa Miwani Akipatiwa maelezo kuhusu kilimo cha Mpunga kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha Mkindo kata ya Hembeti Wilaya ya Mvomero ikiwa ni Maadhimisho ya Siku ya Jumuiya ya wazazi .
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Morogoro  Mh Abdalah Shaweji  Akiwahutubia wananchi wa kata ya Hembeti waliojitokeza kwa wingi katika Sherehe za Umoja wa wazazi Mkoa wa Morogoro Ambapo katika Hotuba yake Aliwataka wana CCM Kushirikiana kwa Pamoja Katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa vitongoji na Vijiji.Pia Alisisitiza Msimamo wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Morogoro ni kwamba Katika Katiba Mpya wanaunga Mkono Msimamo wa Chama cha Mapinduzi wa Serikali Mbili na Kuwaomba wananchi Mara baada ya Rasimu ya Mwisho Kuja waichague serikali Mbili katika Kura ya Maoni ya Kupitisha Katiba Mpya,.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Morogoro  Mh Abdalah Shaweji   Akipanda Miti katika Maazimisho ya Sherehe za Jumuiya ya Wazazi
Wapenzi wa Chama cha Mapinduzi CCM Kutoka Wilaya ya Mvomero wakiwa wamejitokeza kwa Wingi kwenye Maadhimisho ya Siku ya umoja wa Wazazi Kimkoa ambayo Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Morogoro Mh Abdalah Shaweji Alikuwa Mgeni Rasmi kwa niaba ya Mwenyekiti wa Umoja huo.
Wanachama wapya wa chama cha Mapinduzi wakiapa Mbele ya Mgeni Rasmi mara baada ya kukabidhiwa kadi

No comments:

Post a Comment