Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wasioona (TLB) Mwalimu Greyson Mlanga(aliyesimama) akitoa somo juu ya Warsha ya Siku mbili ya Mkatabawa Umoja wa Mataifa Kwa Watu Wenye Ulemavu Mjini Ifakara hivi karibuni. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama Hicho Wilaya ya Kilombero Maria Faya na Kulia ni Mwalimu Janet Kalalu, Mratibu wa Chama Wilaya.
Henry Bernard Mwakifuna, Ifakara-Kilombero
Watu wenye Ulemavu nchini Tanzania wametakiwa kushiriki katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo kwa muuujibu wa Uwezo wao.
Akizungumza katika Warsha ya Siku mbili iliyofanyika Mjini Ifakara Wilayani Kilombero hivi karibuni Mwenyekiti wa Chama cha Wasioona (TLB) Taifa Mwalimu Greyson Mlanga amesema kuwa ni vyema watu wenye Ulemavu wakashiriki katika shughuli hizo ili kusaidia Jamiii kuondokana na Dhana ya kuwa Walemavu ni watu omba omba.
Mwenyekiti huyo amesema kuwa ushirikiano wa Vyama vya Watu wenye Ulemavu ndiyo njia pekee ya kujikwamua katika maisha huku akisisitiza upatikananji wa Takwimu sahihi za Watu wenye Ulemavu ili ziweze kusaidia maendeleo ya Watu wenye Ulemavu.
Katika Mafunzo hayo yaliyoshirikisha wadau mbalimbali wakiwemo Madiwani, Watendaji na Wawakilishi wa Vyama vya Watu wenye Ulemavu, Mwenyekiti huyo alielezea umuhimu wa kupata Elimu na kujua Haki za Watu wenye Ulemavu.
Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Chama cha Wasioona (TLB) Wilaya ya Kilombero yameshirikisha Wadau kutoka Kata za Ifakara, Kibaoni, Kiberege na Kisawasawa yalifadhiliwa na Taasisi ya Foundation for Civil Society.
Viongozi wa TLB Taifa Wakiungana na Viongozi wa TLB Wilaya ya Kilombero katika kuimba Wimbo wa Haki za Binadamu katika Mafunzo ya Siku Mbili yaliyowakutanisha Wadau mbalimbali, Vyama vya Watu Wenye Ulemavu Wilaya ya Kilombero, uliofanyika hivi karibuni Mjini Ifakara. Kutoka Kushoto ni Maria Faya, Mwenyekiti wa TLB Wilaya ya Kilombero Maria Faya, Mwalimu Robert Bundala,Makamu Mwenyekiti Wasioona Taifa, Mwenyekiti wasiona Taifa Mwalimu Greyson Mlanga na Mratibu wa Wasioona Wilaya ya Kilombero Mwalimu Janet Kalalu.
Washiriki wa Mafunzo ya Siku Mbili ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa Juu ya Watu Wenye Ulemavu wakiwa kwenye Picha ya pamoja na Viongozi wa Taifa wa Chama cha Wasiona (TLB) Mjini Ifakara Hivi karibuni.(PICHA ZOTE KWA HISANI YA HENRY BERNARD MWAKIFUNA WA IFAKARA).
No comments:
Post a Comment