Wednesday, April 9, 2014

MBINU MPYA YA KUSAFIRISHA MADAWA YA KULEVYA, WAJAWAZITO WATUMIKA



Baada ya Mambo kuwa magumu kwa wasafirishaji wa madawa ya kulevya, Sasa wamegundua njia mpya ya kusafirisha madawa hayo ya kulevya kwa kuwatumia wajawazito.
Baada ya kugundua kuwa wajawazito hupita bila kukaguliwa na Skana za Viwanja vya Ndege kwa lengo la kumlinda mtoto aliye tumboni kiafya, siku za karibuni wahusika na kitengo cha madawa ya kulevya katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere, wamekamatwa wanawake kadhaa wajawazito ambao miongoni mwao walikutwa wakiwa wamemeza kete za madawa ya kulevya.
Akizungumza kwa njia ya simu kuthibitisha habari hizi Mkuu wa Kitengo cha madawa ya kulevya wa Uwanja wa Julius Nyerere, alisema kuwa walifanikiwa kuwakamata baadhi ya wanawake wajawaziti baada ya kupata taarifa kuwa wamebeba dawa hizo na kuwahuku ambapo baada ya kukaguliwa walikutwa nazo na kuchukuliwa hatua.

''Imekuwa ni vigumu sana kuwakagua wanawake ambao ni wajawazito kutokana na sherika za kiusalama wa kiafya kwa mtoto aliye tumboni kwa mama mhusika, hivyo na wao wamechukulia urahisi wa kutumia njia hiyo kupitisha madawa kwani huwa hawakaguliwi.

Lakini tumeweza kuwakamata baadhi ya wanawake baada ya kupata taarifa za awali na kuwakagua na kuwakuta kweli wakiwa wamemeza kete za dawa hizo na kuwachukulia hatua''. alisema mkuu huyo.

Aidha alisema kuwa njia nyingine inayotumika ni kusafirisha madawa hayo kwa kutumia Cargo ambayo ni mizigo mikubwa ambayo huwekwa nyuma ya ndege chini ama chupa kwa kujaza wakifananisha na maji na wengine husafirisha kama wanasafirisha magunia ya sukari kupeleka Afrika ya Kusini, jambo ambalo liliwashtua wengi wakibaki na mshangao ni vipi sukari isafirishwe kwenda Afrika ya Kusini

No comments:

Post a Comment