Friday, April 4, 2014

RIDHIWANI KIKWETE AKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI,KUZUNGUMZIA MWENENDO WA KAMPENI ZAKE


Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akizungumza na Waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano wake na waandishi hao wakati akizungumzia mwenendo mzima wa Kampeni zake,leo April 4,2014,Nyumbani kwake Msoga.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete.

MGOMBEA ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM), Ridhiwani Kikwete, amesema akipata ridhaa ya wananchi, atahakikisha anajenga stendi ya mabasi na soko ili kutoa fursa kwa vijana kupata eneo la kuuzia bidhaa zao.


Ridhiwani amesema nia ni kuhakikisha vijana wanaouza bidhaa za vinywaji na zingine waweze kuwauzia abiria wa mabasi yatakayowekewa masharti ya kuingia stendi.


Akizungumza katika mkutano wake na Waandishi wa habari alipokuwa akielezea mwenendo mzima wa Kampeni zake, Ridhiwani amesema kiu yake ni kuona vijana wanapata masoko ya uhakika ya bidhaa zao.


Amesema atashirikiana na  madiwani wa halmashauri kutafuta eneo nzuri la kujenga stendi na soko hilo litasaidia kuinua jimbo la Chalinze kiuchumi.


“Nimesikia watu wanasema kuhamishwa kwa mizani ya Chalinze , vijana watakosa mahali pa kufanyia biashara zao.Kimsingi mizani si eneo la kufanyia biashara kwanza mabasi yanasimama muda mfupi lakini suluhisho ni stendi,”alisema



Alisema lengo ni kuhakikisha wanatumia fursa ya kuwa njia panda ya mikoa ya Kaskazini na Nyanda za juu Kusini na mikoa ya Kati , kuhakikisha kunakuwa na soko la uhakika.

No comments:

Post a Comment