Na Magreth Kinabo –Dodoma
Imeelezwa muundo wa Serikaili tatu unaweza kusababisha kudhoofisha Muungano, kuongeza gharama za uendeshaji na utaleta athari za kiuchumi.
Hayo tamebainishwa katika kitabu cha KATIBA BORA TANZANIA kilichoandikwa na wanataaluma 100 kutoka Taasisi ya Utafiti ya Vyuo Vikuu vya nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika(ESAURP), ambacho kilikabidhiwa leo kwa Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samia, Suluhu Hassan na Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo, Profesa Ted Maliyamkono mjini Dodoma.
Wanataaluma hao katika kitabu hicho kupitia hitimisho la baadhi yao,ambao ni Profesa Ted Maliyamkono, Dk. Hugh Mason na Profesa Bonaventure Rutinwa.
Akizungumzia kuhusu Urai na Haki za Kiraia kulingana na Rasimu ya Katiba mpya inayopendekezwa wakati wa ufafanuzi wa kitabu hicho kwa Makamu Mwenyekiti huyo wa Bunge hilo, Profesa Rutinwa anasema suala la serikali tatu linaweza kuwa na athari hasi.
Profesa Rutinwa anasema rasimu hiyo ifanyiwe marekebisho kwa ajili ya kuhakikisha wananchi wote wanafurahi kupata haki za kijamii na za kiuchumi katika Jamhuri ya Muungano ikiwa ni pamoja na uhuru wa kutembea, haki ya kufanya kazi na kupata rasilimali kama vile ardhi na masoko.
“ Hata hivyo tafiti juu ya vifungu vingine vya rasimu ya Katiba vinaonesha kwamba madhara ya muundo wa serikali tatu yanazidi faida zilizotolewa, kwa hiyo pendekezo la kubakiza muundo wsa serikali mbili litakuwa na manufaa zaidi na hivyo ni vema pendekezo hii likapewa uzito wa kipekee,” anasema Profesa Rutinwa katika hitimisho la mada yake kwenye kitabu hicho.
“Muundo wa Serikali tatu uliopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba unaweza kuwa na faida katika suala la uwakilishi wa kidemokrasia, unaweza kuhatarisha Mustakabali wa Jamhuri ya Muungano kwani kuendelea kugawanywa kwa Serikali ya Muungano kunaweza kudhoofisha Muungano,” walisema wasomi hao.
Aidha wasomi hao walifafanua kuwa mshikamano wa nchi unaweza pia kuhatarishwa kwani masuala yenye utata yanaweza kuchuakua sura tofauti katika nchi mbili za Muungano, na hivyo kusababisha mvutano mkubwa.
Akizungumzia kuhusu tafsiri ya kiuchumi na kifedha kuhusu Muungano wa Serikali mbili na Serikali tatu, Profesa Nehemiah Osoro ambaye ni mtaalamu wa uchumi anasema gharama za kuendesha Muungano wa Serikali tatu zinaweza kuwa ni kubwa ambazo zisizoepukika zinazohusiana na uamauzi wa Serikali tatu, badala ya mbili.
“ Muundo wa Serikali tatu unaweza kufaa kwa mtazamo wa kisiasa ,lakini hauifai kwa mtazamo wa kiuchumi,” anasema.
Aliongeza kuwa muundo wa sasa wa Muungano ni bora kiuchumi kuliko ule unaopendekezwa. Hivyo mamlaka ya kisiasa huwa bora panakuwa na mamlaka ya kiuchumi.
Profesa Osoro akizungumzia kuhusu gharama za kuendesha mfumo wa Serikali tatu wenye nchi huru mbili yaani Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali Shirikisho.
Anaongeza kuwa Tanzania Bara ni nchi kubwa na tajiri kwa madini na rasilimali nyingine za asili, hivyo inaweza kugharamia matumizi yake yote na kuchangia sehemu ya mapato yake katika Serikali ya Muungano, wakati Zanzibar ni nchi ndogo na idadi ya watu wasiopungua milioni na rasimali chache, mbali na utalii ni dhaifu kiuchumi.
Profesa huyo anaeleza kuwa kwa Tanzania kuwa tajiri katika rasilimali na idadi ya watu, inaweza kubeba gharama za kuendesha Muungano uliopo. Hivyo Tangu mwaka 1968 ,Serikali ya Zanzibar haijatoa mchango wa uendeshaji wa Serikali ya Muungano. Inapata asilimia 4.5 ya msaada inayopokelewa na Serikali ya Muungano.
“ Kama muundo wa Serikali tatu utapitishwa,Zanzibar itabeba gharama zote za Serikali yake, ambazo zitakuwa kuliko ilivyo sasa kutokana na kuhamishwa kwa baadhi ya majukumu ya kutoka ngazi ya shirikisho kwenda katika ngazi ya nchi, itatakiwa kugharamia mambo 15 ya Muungano, ambayo yameondolewa kutoka katika mambo ya sasa,” alisisitiza.
Mtaalum huyo wa uchumi anahoji kuwa Zanzibar imeshindwa kuchangia sehemu ya mapato yake katika Serikali ya Muungano. Kama hilo likitokea sasa je itaweza kuchangia fedha katika Muungano unaopendekezwa?
“ Kiuchumi ,Zanzibar iko vizuri ikibakia kwenye Muungano wa sasa. Kama Zanzibar itashindwa kuchangia sehemu iliyotengewa, ambalo linaweza kutokea, hii itakuwa chanzo cha migogoro na migongano na inaweza baadaye kusababisha kuvunjika kwa Muungano,” anasema Profesa Osoro huku akiongeza uwezo wa Zanzibar katika kuchangia utaimarishwa na kuondolewa kwa ushuru wa forodha.
Anaendelea kuchanbua kuwa Bajeti ya Zanzibar kwa mwaka inakaribia Sh. bilioni 650.Ikiwa Zanzibar itatakiwa kuchangia asilimi 10 ya gharama za kuendesha serikali ya Shirikisho(kiasi cha Sh. bilioni 100 itakuwa ni sawa na kuchangia asilimia 15 ya bajeti yake kwa mwaka katika Serikali ya Muungano.
Hivyo Serikali ya Zanzibar ingekuwa na upungufu wa Sh. bilioni 100, ikitokea ikashindwa kuchangia sehemu yake, Tanzania Bara haitakubali kwa ina iwezo wa kujitegemea.
“ Hii itasababisha mgogoro na misuguano,ambayo hata inaweza kusababisha kuvunjika kwa Muungano,” anasisitiza.
Anasema kwa sasa nusu ya Wazanzibar wanaoishi katika Tanzania Bara, baadhi yao ni wafanyakazi, wengi ni wafanyabiashara na wawekezaji, mambo yanaweza kuwa tofauti wakirudishwa kwao kutokana na muundo wa serikali tatu(Shirikishi).
HIvyo inawezakuwa na athari uchumi wa visiwani kwa sababu ya kupunguakwa mapato ambayo walikuwa wanachuma Bara
No comments:
Post a Comment