Jeneza likiwa na mwili wa aliyekuwa Askofu wa kanisa la Anglican
Dayosisi ya Dodoma Godfrey Mdimi Mhogolo aliyefariki wiki iliyopita
nchini Afrika ya Kusini alikopelekwa kwa matibabu likiwa ndani ya kanisa
kuu la Roho Mtakatifu wakati wa ibada maarumu.
Waumini na viongozi wa kanisa la Anglican Dayosisi ya kati wakilishusha
Jeneza lilibeba mwili wa aliyekuwa askofu wa kanisa hilo Godfrey Mhogolo
ulipofikishwa kwa mara ya kwanza tokea alipofariki nchini Afrika ya Kusini kanisani hapo kwa ajili ya kufanyiwa ibada ya maombezi.
Wachungaji na makasisi wa Kaanisa la Anglican Dayosisi ya Kati wakiwa
wamejipanga nje ya kanisa la Roho mtakatifu mjini Dodoma kwa ajili ya
kuupokea mwili aliyekuwa Askofu wa kanisa hilo Godfrey Mhogolo.
Waumini wa kanisa la Anglican wakiwa kwenye mahema yaliyowekwa nje ya
kanisa kuu la Roho Mtakatifu walipokuwa wakifuatilia ibada ya kuuombea
mwili wa aliyekuwa Askofu wa Kanisa hilo kanda ya Dodoma aliyefariki
wiki iliyopita alipokuwa kwenye matibabu nchini Afrika ya Kusini.
Wageni mbalimbali kutoka nje ya nchi wakiwa ndani ya kanisa la Roho
Mtakatifu kwa ajili ya ibada maaumu ya kuuombea mwili liyekuwa askofu
wa kanisa hilo Godfrey Mhogolo aliyefariki wiki iliyopita alipokuwa
kwenye matibabu Afrika ya Kusini.
Ndani ya kanisa la Roho mtakatifu waumini wakifuatila ibada ya kuuombea
mwili wa aliyekuwa askofu wa kanisa hilo Godfrey Mhogolo aliyefariki
wiki iliyopita akiwa kwenye matibabu.
Baadhi ya Viongozi wa Serekali wakiwa kwenye ibada hiyo.
Waumini wa kanisa hilo wakiwa ndani ya hema lilijengwa katika eneo la
makaburi ya kuzikia viongozi wa kanisa la Anglican Dayosisi ya kati
ambapo walikuwa wakiandaa sehemu ya kuuzikia mwili wa aliyekuwa Askofu
wa Kanisa hilo Godfrey Mhogolo unaotarjiwa kuzikwa kesho Jumamosi.
PICHA NA JOHN BANDA WA PAMOJA BLOG
No comments:
Post a Comment