Kikosi cha TSN Boys
TIMU ya soka
ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) inashuka dimba la Sigara, Chang’ombe, Dar es Salaam kuikabili Mwananchi katika Kombe la NSSF kwa Vyombo
vya Habari 2014.
Mechi hiyo
itakayochezwa saa 2 asubuhi, itakuwa muhimu kwa timu zote mbili kwani mshindi
atasonga mbele katika hatua ya robo fainali zitakazoanza Jumatatu ijayo.
TSN imetinga
hatua hiyo baada ya kupewa ushindi kutokana na wapinzani wao, Mlimani Media
kuwatumia wachezaji ambao hawakuwa halali. Mlimani Media ilikuwa imeshinda kwa
mabao 9-0.
Mwananchi ni
mechi yake ya kwanza. Mbali ya mechi hiyo, mechi nyingine kesho ni kati ya
Tumaini dhidi ya Sahara Media, wakati upande wa netiboli, itakuwa ni mechi za
robo fainali kati ya Business Times dhidi ya Shirika la Utangazaji Tanzania
(TBC), wenyeji NSSF dhidi ya Tumaini Media.
TSN Boys wapo katika hamasa na ari kubwa ya mchezo huo wa kesho ambapo Meneja wa Timu hiyo, Mroki Mroki "Father Kidevu" ameahidi kuzawadia mfungaji wa kila goli kitita cha shilingi 5,000.
"Niliahidi katika mchezo wa awali na hata sasa bado ahadi yangu ipo pale pale kwa kila goli nitalilipia shilingi 5,000 nahiyo haina longolongo lengo ni kuhamasisha ushindi kwa timu yetu," alisema Mroki.
Aidha Mroki amesema atakuwepo uwanjani kuhakikisha ushindi unapatikana kwa vijana wa TSN Boys na kusonga mbele katika mashindano hayo.
Katika mechi
za jana, mabingwa watetezi wa soka, Jambo Leo walitolewa baada ya kufungwa mabao
2-1 na Free Media kwa mabao ya Saleh Mohammed.
Bao la Jambo
Leo lilifungwa na Zahoro Mlanzi. Aidha, Changomoto ilisonga mbele baada ya
kuilaza New Habari kwa penalti 7-6, baada ya sare ya bao 1-1. Free Media na New
Habari zilisonga mbele kama timu bora mbili zilizoshindwa, lakini zikiwa na matokeo
mazuri (best looser).
Katika
netiboli, Mlimani Media ilishindwa kutamba kwa Habari Zanzibar kwa kufungwa mabao
19-15, wakati IPP iliizamisha Global Publishers kwa
mabao 27-8.
No comments:
Post a Comment