Friday, June 14, 2013

*WA IVORY COAST WATUA BONGO BILA DROGBA KUIKABILI STARS JUMAPILI

 Mchezaji wa timu ya Taifa wa Ivory Coast, anayekipiga na chama la Man City, jijini London, Yaya Toure, akiwasali na wenzake kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana jioni, tayari kwa ajili ya kuwakabili Timu ya Taifa 'Taifa Stars' mchezo utakaochezwa siku ya Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ikiwa ni mchezo wa kuwania kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia 2014, nchini Brazil. Timu hiyo baada ya kuwasili Dar imeweka Kambi katika Hoteli ya Bahari Beach nje kidogo ya Jiji la Dar.
 Solomon Kalou (kushoto) na Bakari Kone, wakiwasili......Timu hiyo imewasili bila mshambuliaji wake wa kimataifa, anayekipiga na chama la Galatta Salay ya Uturuki, Didier Drogba.
Mchezaji wa Arsenal, Gervinho, akitua katika ardhi ya Bongo......Picha kwa hisani ya Bin Zubeir

No comments:

Post a Comment