Monday, June 17, 2013

*BENKI YA NMB YA ZINDUA CHAP CHAP AKAUNTI KWA AJILI YA WATANZANIA WASIO NA AKAUNTI

Benki ya NMB imeendelea kuwa kinara katika kubuni na kuboresha huduma mbali mbali za kibenki, ili kuwawezesha wateja wake kupata unafuu na urahisi wa upatikanaji wa huduma za kibenki nchini Tanzania. 

Katika kulizingatia hili mwishoni mwa wiki Benki  ya NMB ilizindua akaunti ya Chap Chap ambayo kusudi kubwa ni kuwafikia wananchi wote kule waliko na kuwafungulia akaunti zao.


Kikubwa zaidi ni kwamba mteja ataweza kufungua akaunti papo hapo na kupata kadi yake ya kutolea fedha  ndani ya dakika  kumi
·         
Mambo muhimu zaidi ambayo mteja wa Chap Chap anaweza kufaidika nayo ni pamoja na kuona salio la akaunti yako popote ulipo.
Mh. Waziri wa fedha Dk William Mgimwa akichukuliwa alama za vidole na Ofisa mauzo ya Nje NMB Abdul Kandoro mara baada ya uzinduzi rasmi wa NMB chap chap akaunti mwishoni mwa wiki mkoani Dodoma.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Mark Wiessing akimshukuru Mh. Waziri wa Fedha Dk. William Mgimwa mara baada ya kuzindua akaunti ya NMB Chap chap.

Baadhi ya maofisa wa NMB na wageni waalikwa kwenye uzinduzi huo

No comments:

Post a Comment