Saturday, June 15, 2013

"ANAKONDA" LADY JAY DEE NI NOMA


 Hivi ndivyo hali ilivyokua ndani ya Ukumbi huu wa Nyumbani Lounge,Namanga jijini Dar es Salaam ambapo bonge moja la show la Mwanadada mkongwe kwenye tasnia ya muziki hapa nchini,Lady Jay Dee ambaye anatimiza miaka 13 tangu alipoanza kazi yake ya muziki.katika show hii wanamuziki mbali mbali walipanda jukwaani akiwepo Mh. Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini,Mh. Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu.
 Wadau mbali mbali wa muziki hapa nchini wakiwa ndani ya ukumbi nyumbani  lounge kushuhudia show ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu na wapenzi wa muziki.
 Ndani ni nyomi la hatari,lakini nje nako watu bado wanataka kuingia huku wengi wao wakisema kuwa "hata kama hakuna siti,sie tuko radhi kusimama ilimradi tumsapoti Dada yetu.
 Getini mambo yako namna hii.
Cheki ndani kumejaa lakini watu bado wamepanga folen.
Burudani ya Utangulizi ikiendelea.

No comments:

Post a Comment