Friday, June 14, 2013

TARATIBU ZA MAZISHI YA MSANII LANGA INAFANYIKA MIKOCHENI


 Mipango ya mazishi ya msanii wa muziki wa Hip Hop, Langa Kileo inafanyika nyumbani kwao Mikocheni mtaa wa Ursino jijini Dar es Salaa, Msanii huyo wa wa Hip Hop alifariki dunia Juni 13 katika hospitali ya muhimbili jijini Dar es Salaam. Akizungmza na Clouds Fm, Ofisa Uhusiano wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Ameniel Aligaesha, amethibitisha kwamba msanii Langa, amefariki majira ya saa kumi na moja za jioni, baada ya kufikishwa hospitalini hapo juzi jioni.

Hata hivyo uongozi wa Muhimbili hauna uwezo wa kusema kilichomuua Langa, kutokana na maadili ya kazi zao, bali ndugu wa  marehemu. Kifo cha Langa kitokea ikiwa ni siku 17 tangu kufariki kwa msanii mwingine wa Hip Hop na Freestyle Master, Albert Mangwea A.k.a Ngwea.

Mungu ailaze roho ya matehem mahali pema peponi

No comments:

Post a Comment